Al Ahly ya Misri wametwaa taji la Ligi ya Mabingwa wa Afrika kwa mara ya 12 kufuatia ushindi wao wa 1-0 dhidi ya Esperance ya Tunisia, katika mchezo wa fainali uliofanyika Jumamosi, Mei 25, 2024.
Awali, katika mchezo wa kwanza uliofanyika katika uwanja wa kimataifa wa Cairo, kiungo wa Esperance Roger Aholou alijifunga, na hivyo kuwapa faida Al Ahly.
Kwa upande wao Esperance ya Tunisia, imeshinda taji hilo la CAF katika miaka ya 1994, 2011, 2018 na 2019.
TRT Afrika