Kenya, Uganda na Tanzania wametangazwa rasmi kuwa waandaaji wa Kombe la Taifa Bingwa Afrika Afcon 2027.
Nchi hizo zilitangazwa Jumatano, na Shirikisho la Soka Afrika CAF, katika hafla fupi iliyofanyika mjini Cairo nchini Misri.
''Naomba kusisitiza kuwa ninajivunia sana matokeo ya leo,'' amesema Rais wa Shirikisho la Soka Afrika Dr Patrice Motsepe.
''Hata hivyo nayapongeza mataifa yote yaliyowasilisha maombi yao hata kama hawakushinda zabuni hii, kwani kwa mtazamo wangu wote ni washindi,'' aliongeza Dkt. Motsepe.
"Ukitazama jinsi walivyowasilisha ombi lao, unaona marais wote wa nchi hizo, Rais Ruto, Rais Samia na Rais Museveni wote walionesha kujitolea kikamilifu kufaniskisha kombe hilo," alisema Dkt Motsepe.
Nchi hizo za Afrika Mashariki ziliwapiku wagombea wenza, Senegal, Botswana na Misri.
''Tutakuwa wakali sana kuhusu suala la mahitaji ya maandalizi ya kombe hilo kwa nchi hizi, ikiwemo kuhakikisha usafiri mwepesi wa kuingia na kutoka kati ya nchi hizo, miundombinu na ushirikiano wa jumla.''
Kinachofuatia sasa amesema Dkt Motsepe ni hakikisho la kufuatwa kwa kanuni zote na maandalizi yakamilike katika muda unaotakiwa.
''Tutakuwa wakali sana kuhusu suala la mahitaji ya maandalizi ya kombe hilo kwa nchi hizi, ikiwemo kuhakikisha usafiri mwepesi wa kuingia na kutoka kati ya nchi hizo, miundombinu na ushirikiano wa jumla,'' Dr Motsepe amesema.
Pia Shirikisho la CAF limesema litaanza kuwatuma wajumbe wake katika nchi hizo tatu kufuatilia maandalizi yao na kutoa usaidizi mwingine wowote unaohitajika.