Nafasi 9 zimetengewa timu za Afrika katika kombe la Dunia 2026 Picha : Twitter CAF 

Tanzania wamepewa mtihani mgumu kuwekwa pamoja na washiriki wa kombe hilo mara 6 Morocco katika droo ya kuwatafuta wawakilishi wa Afrika katika Kombe la Dunia 2026.

Morocco wanatazamiwa kuwa nyota wa Afrika kwa kuwa timu ya pekee Afrika kufika nusu fainali ya shindano hilo la kimataifa.

Wengine katika kundi lao ni Zambia, Congo, Niger na Eritrea.

Kenya kwa upande wake wamewekwa kundi moja na mabingwa mara mbili wa kombe lataifa bingwa Afrika Cote D'Ivore. Wengine watakaopambana nao katika kundi hili ni Gabon, Gambia, Burundi na Seychelles.

Afrika imetengewa nafasi 9 katika kombe la Dunia 2026.

Misri walioshinda ubingwa wa Afrika Afcon mara 7, nyingi zaidi kuliko taifa lingine lolote wamejikuta pamoja na Burkina Faso, Guinea-Bissau, Ethiopia, Sierra Leone na Djibouti.

Awamu ya makundi katika kombe la dunia 2026 imefanyiwa mabadiliko kuwa makundi 12 ya timu 4 kila moja Picha Twitter CAF

Vigogo Nigeria ambao wamefuzu mara 6 kati ya mitanange 8 ya Kombe la Dunia zilizopita, watamenyana na Afrika Kusini, Benin, Zimbabwe, Rwanda na Lesotho katika Kundi C.

Kwa mara ya kwanza kombe la Dunia litakutanisha timu 48 Picha Twitter CAF

Uganda nao wamo katika kundi G inayoongozwa na mibabe Algeria na Guinea. Wengine katika Kundi hili ni Somalia, Botswana, Msumbiji, na Guinea.

TRT Afrika