FIFA itaadhimisha miaka 100 ya shindano hilo katika kombe la 2030 litakaloanaliwa kwa pamoja na Morocco, Uhispania na Ureno./ Picha : Reuters  

FIFA ilisema Jumatatu ilipokea huko Paris maombi rasmi vya zabuni kutoka kwa viongozi wa mashirikisho saba wanachama ambao ndio wazabuni wa kipekee wa Kombe la Dunia la 2030 na 2034.

Kombe la Dunia la 2030 linaandaliwa kwa pamoja na Uhispania, Ureno na Morocco huku nchi tatu za Amerika ya Kusini - Argentina, Paraguay na Uruguay wakipewa fursa kuandaa mechi tatu kama maadhimisho ya maiaka 100 ya kombe hilo ambalo lilichezwa kwa mara ya kwanza nchini Uruguay 1930.

Saudi Arabia ndio mgombea pekee wa kuandaa Kombe la Dunia la 2034 waliowasilisha nia yao kwa FIFA kufikia mwisho wa 2023.

Zabuni hizo mbili zimepangwa kuthibitishwa katika mkutano wa mtandaoni wa Desemba 11 wa mashirikisho 211 wanachama wa FIFA.

Lazima wazabuni hao waonyeshe wazi mipango ya miradi inayopendekezwa ya Kombe la Dunia ambazo lazima ijumuishe mipango ya viwanja, hoteli, viwanja vya mazoezi, usafiri na usalama wa taifa.

"FIFA itatathmini kwa kina vitabu vya zabuni na kuchapisha ripoti yake ya tathmini" katika robo ya mwisho ya mwaka, shirikisho la soka duniani lilisema katika taarifa.

Sera ya FIFA ya haki za binadamu

Wazabuni wa Kombe la Dunia pia lazima sasa wakubali kufanyiwa tathmini ya wajibu wao wa haki za binadamu kuandaa mashindano hayo. FIFA ilialikwa mwezi Mei kufanya kazi na wataalamu huru kutathmini wagombeaji.

Sera ya FIFA ya haki za binadamu ilianzishwa miaka minane iliyopita baada ya kutoa matoleo ya 2018 na 2022 kwa Urusi na Qatar, mtawalia, na ilitumika kwa mara ya kwanza kwa wagombeaji wa mashindano ya 2026.

Marekani, Canada na Mexico watashirikiana kuandaa Kombe la Dunia la 2026, la kwanza likiwa na timu 48 badala ya 32. Walishinda mzabuni hasimu wao Morocco kwa kura 134-65 iliyoamuliwa mwaka 2018 mjini Moscow.

TRT Afrika na mashirika ya habari