Tuzo la wachezaji wa Africa / Photo: Reuters

Shirika la Soka la Kongo (Fecofa) limetoa madai kwa Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) kuhusu baadhi ya maamuzi ya usuluhishi wakati wa mechi ya mkutano wa mwisho la timu ya taifa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) dhidi ya Mourabitounes ya Mauritania

Mechi ambayo ni ya raundi ya nne ya kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika (CAN), Ivory Coast 2023.

Hatua hii ya shirikisho la soka kutaka mechi irudiwe ndio mwitiko ambao wafuasi wa soka nchini Kongo walikua wanataka ufanyike.

Miongoni mwa sababu zilizosababisha wafuasi wasoka kulalamika ni kuondolewa kwa mchezaji Cédric Bakambu katika hatua ya kutatanisha.

Pia shirikisho hilo la soka DRC lilimshutumi Mwamuzi wa Tunisia Selmi Sadok kwa kutoa kadi nyekundu kwa Bakambu bila kujiridhisha kwenye tekinolojia ya VAR.

Timu hiyo ya taifa ya Congo, Leopard ilikuwa inaongoza kwa bao moja na punde baada ya kutolewa mchezaji mwenzao Mauritania ikarejesha goli na wakahitimisha mchezo kwa mabao (1-1)

Hata hivyo timu hiyo ya taifa ya Congo bado wako kwenye kinyang'anyiro cha kufuzu baada ya kuchukua pointi 4 mbele ya Mauritania.

TRT Afrika na mashirika ya habari