Wachezaji wa Misri wakishangilia na kikombe baada ya ushindi wao wa 1-0 wa Fainali ya AFCON kati ya Cameroon na Misri Uwanja wa Ohene Djan mjini Accra, Ghana. (Picha na Lee Warren/Gallo Images/Getty Images)

Je, unafahamu baadhi ya rekodi za kuvutia na takwimu za kombe la AFCON?

  • Makala ya AFCON 2023 Cote d ' Ivoire ni ya 34 ya mashindano hayo tangu yalipoanzishwa rasmi mnamo 1957.

  • Cote d ' Ivoire ni mwenyeji wa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Mara ya pili, walikuwa wenyeji wa mashindano hayo kwa mara ya kwanza mwaka 1984.

Afcon 2027

  • Nchi 15 bora Afrika zimefuzu kushiriki dimba la Kombe la Mataifa bora Afrika 2023.

  • Misri ndio timu iliyotwaa mataji mengi ya Afcon (7), ikifuatiwa na Cameroon (5), Ghana (4), Nigeria (3), Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (2) na Ivory Coast (2).

  • Kocha wa Senegal Aliou Cisse ndiye mtu wa kwanza kupoteza katika fainali za Afcon kama mchezaji (2002) na akiwa kocha (2019).

  • Mkameruni Samuel Eto'o ndiye anayeshikilia rekodi ya mfungaji bora wa Jumla wa Kombe la Mataifa bora Africa, Afcon, akiwa na mabao 18 kupitia mashindano sita kati ya mwaka 2000 na 2010.

Samuel Eto'o

  • Samuel Eto'o wa Cameroon, Asamoah Gyan pamoja na Andre Ayew wa Ghana na Kalusha Bwalya wa Zambia pekee ndio nyota wanne pekee waliofunga mabao katika makala 6 ya mashindano ya AFCON zaidi ya wengine.

  • Golikipa mstaafu wa zamani wa misri Essam El Hadary ndiye mchezaji mzee zaidi kuwahi kuonekana kwenye mashindano hayo alipocheza akiwa na umri wa miaka 44 na siku 21 akiwa katika kikosi cha Misri dhidi ya Cameroon katika fainali ya 2017 huko Libreville wakati Misri ilipopoteza.

  • AFCON imepanuliwa kutoka timu 16, hali iliyokuwa kati ya1996 hadi 2019 wakati mashindano hayo yalipobadilishwa na kuwa na timu 24 mnamo 2019.

Kombe la washindi linabebwa uwanjani baada ya mechi ya Fainali ya AFCON kati ya Cameroon na Misri kwenye Uwanja wa Ohene Djan mjini Accra, Ghana. | Picha: Getty

  • Mfaransa Herve Renard ndiye kocha pekee aliyewahi kushinda AFCON akiyaongoza mataifa mawili tofauti; alipoisaidia Zambia mnamo 2012 na Cote D'ivoire mwaka 2015.

TRT Afrika