Nigeria yaishinda Afrika Kusini kufika fainali ya Afcon

Nigeria yaishinda Afrika Kusini kufika fainali ya Afcon

Mechi ya nusu fainali ilimalizika 1-1 baada ya muda wa ziada
William Troost-Ekong wa Nigeria akishangilia baada ya kufunga bao lake la kwanza. Picha / Reuters

Mchezaji mbadala (substitute) Kelechi Iheanacho alifunga kuwapa ushindi Nigeria wa penalti 4-2 dhidi ya Afrika Kusini siku ya Jumatano baada ya mechi ya kusisimua ya nusu fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika huko Bouake.

Mechi hiyo ilimalizika 1-1 baada ya muda wa ziada na mabingwa mara tatu watakutana na wenyeji Ivory Coast au Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika fainali siku ya Jumapili.

TRT Afrika