Alishawahi kuwa kwenye chumba cha kubadilishia nguo cha Muhammad Ali, akijitayarisha kwa moja ya pambano lake maarufu.
Amekumbana bega kwa bega na Pele ambaye alichambua na kusimulia maisha yake katika taaluma ya soka ya kulipwa.
Alifuatilia maisha ya mwanariadha maarufu wa Kenya Kipchoge Keino tangu alipokuwa mwanariadha chipukizi hadi kubadilika kwake kama mwanariadha bora duniani.
Katika safari hiyo , miaka 60 tangu sakata kuanza kwake , Orhan Ayhan wa Uturuki mwenye umri wa miaka 85 amefikia kilele cha rekodi ambayo itakuwa yake mwenyewe - kutambuliwa na Gkumbukumbu ya Guinness kama ripota na mchambuzi wa michezo aliyekaa muda mrefu zaidi katika taaluma hiyo.
Safari ya Orhan inavutia na kusisimua sawa na magwiji wa michezo ambao majina na kumbukumbu zao zipo akilini mwake na hutamka kwa wepesi kutokanana uzoefu wake nao.
Anakumbuka vizuri jinsi mabadiliko kutoka kwa kuripoti hadi uchambuzi juu ya michezo yalifanyika bila yeye kutarajia.
"Ilikuwa baridi sana siku hiyo, nakumbuka," Orhan anasimulia TRT Afrika, akirejelea tukio la miongo mitatu nyuma. "Safari za ndege zililazimika kughairishwa, na kulikuwa na theluji kila mahali."
Kwa mbali, sauti kubwa za maelfu ya mashabiki wa soka zilisikika kupitia Uwanja wa Dolmabahçe wa Istanbul, ambao sasa unajulikana kama Besiktas au Vodafone Arena.
Uwanja huo ulikuwa mwenyeji wa robo fainali ya klabu bingwa Ulaya. Orhan, ripota wa michezo kwa karibu miaka 30 kufikia wakati huo, hakuwa na wazo kwamba maisha yake yangebadilika milele.
"Tayari nilijulikana kama ripota wa michezo, nikifanya kazi na gazeti la ndani liitwalo Tercuman Gazette," anakumbuka. "Waliniorodhesha miongoni mwa wachambuzi wengine wanne, ambao wote walikuwa na majina makubwa wakati huo. Nilikuwa na wasiwasi."
Orhan hakuruhusu wasiwasi kumvunja moyo, akiangalia fursa badala yake kama ambayo inaweza kumpeleka kwenye mambo makubwa zaidi.
“Tulitakiwa kila tufanye uchambuzi wa mchezo huo kwa zamu kwa dakika 15 kila mmoja, mimi nilikuwa wa pili kwenda, na nilipoanza hata mabosi hawakutaka nisitishe, najua sana soka, unaona. - hivyo ndivyo nilivyowashinda wengine!" Anasema.
Maisha magumu ya mwanzoni
Uso wa Orhan unang'aa anapokumbuka umbali ambao amesafiri. Alizaliwa Januari 1938 kama mkubwa kati ya ndugu watatu, maisha ya awali ya Orhan yalikuwa magumu kwani baba yake - mkufunzi wa michezo katika klabu ya eneo hilo - alijitahidi kupata riziki.
"Nilidhamiria kuisaidia familia yangu, na michezo ndiyo ilikuwa chombo changu. Nilipenda kitu chochote kinachohusiana na michezo, ikiwa ni pamoja na mpira wa miguu, ambao nilicheza na timu za jirani. Pia nilicheza mpira wa kikapu na ngumi, ambao nilipenda," anasema. "Kwa namna fulani, nilijua kwamba mchezo ungenisaidia kupata maisha bora."
Moja kwa moja hadi miongo sita baadaye, Orhan ana kitabu cha kumbukumbu cha maisha yake kama mchambuzi, chenye hsitoria ya zaidi ya matangazo 15,000 katika soka na ndondi, miongoni mwa mafanikio mengine.
Kazi yake imempeleka katika mabara matano kuangazia baadhi ya matukio makubwa zaidi katika michezo.
"Kama shabiki wa ndondi, huwezi kusahau kukumbuka Oktoba 30, 1974?" anasema, uso wake ukionyesha msisimko wa kuzungumza juu ya kauli maarufu ya "Rumble in the Jungle".
"Mabingwa wawili nguli wa uzito wa juu wakiwa ulingoni pamoja. Sikuwa na jinsi ningeweza kukosa hilo," anasema kuhusu pambano la Muhammad Ali-George Foreman. "Nilishangaa."
Orhan alisafiri kwa ndege hadi Zaire, ambayo sasa ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ili kushuhudia kile kilichoingia katika historia kama tukio kubwa zaidi la ndondi kuwahi kutokea.
Hili halikuwa jambo lake pekee maarufu na Afrika. "Pia nimepata fursa ya kuripoti kuhusu Kipchoge Keino, mwanariadha maarufu. Nimeona kazi yake tangu alipokuwa kijana hadi kufika sehemu ambayo amevunja rekodi," anakumbuka.
Orhan aliendelea na michezo sita ya Olimpiki. Sauti yake maarufu pia ilipamba kisanduku cha maoni kwenye Kombe kadhaa za Dunia za mpira wa Miguu. Amefanya kazi kwa karibu kila jumba la habari na uchapishaji huko Uturuki, akiripoti, kuhariri, kuandika habari, na kutoa maoni kwa miaka mingi.
Tarehe 3 Juni 2016, imewekwa katika kumbukumbu ya Orhan kama siku ya huzuni kwa michezo na kibinafsi. Hiyo ndiyo siku aliyofariki Muhammad Ali.
"Nilimfuata mtu huyu katika maisha yake yote, nikijenga, uhusiano ambao Unakaribia kuhisi kama wewe na yeye marafiki," asema.
Wakati nguli huyo wa ndondi mwenye umri wa miaka 74 alipotangazwa kufariki katika hospitali moja huko Phoenix, Arizona, jambo ambalo halikutarajiwa lilitokea katika maisha ya Orhan.
"Nilipokea simu. Rais Recep Tayyip Erdogan akitangaza habari za kifo cha Ali kwenye gari lake. Alikuwa shabiki. Na alijua mimi ni shabiki mkubwa. Aliwaomba watu wake wanipigie simu na kupanga safari yangu ya Marekani kuhudhuria mazishi."
Orhan anahesabu hii kama moja ya nyakati hizo za uchungu maishani mwake. Ingawa alikuwa na furaha kwamba Rais Erdogan alikuwa ametambua kazi yake kwa miaka mingi, kilele cha safari yake kuhusu maisha ya Muhammad Ali kilikuwa ni kiashiria mwisho wa enzi.
Siku chache baadaye, Orhan alijikuta kwenye msafara wa Rais Erdogan kuhudhuria mazishi ya Mohammed Ali. "Wakuu wa nchi, watu mashuhuri, viongozi wa haki za kiraia, waigizaji wa sinema ... kulikuwa na watu wengi wakubwa huko," anasema juu ya mkusanyiko wa watu waliojitokeza.
Katika kazi yake yote, Orhan ameshuhudia rekodi zikivunjwa.
Sasa, ni wakati wa kusherehekea urithi wake kwani miaka 60 ya kutoa maoni na kuripoti inamweka sawa na mmiliki wa sasa wa rekodi ya dunia ya Guinness kwa kazi ya muda mrefu zaidi kama ripota wa michezo, marehemu György Szepesi wa Hungary, ambaye alishinda taji hilo. 2006.
Orhan atachukua nafasi hiyo baada ya miezi michache anapotimiza miaka 61 katika taaluma yake. "Siangazii sana hilo kwa sasa," anaiambia TRT Afrika. "Kwa umri wangu kila kitu ni baraka, namshukuru Mungu kila siku ninapoamka nikiwa na afya njema na kuendelea kufanya kile ninachokipenda. Ikimaanisha nivunje rekodi nitashukuru, tuone kitakachotokea."
Mtoto wa Orhan, Korhan Ayhan, anaomba na kuhesabu miezi minne iliyosalia kwa kile ambacho kitakuwa ushindi mkubwa isiyo na kifani kwake. Hesabu kufikia miaka 61 ya utangazaji imeanza.