Angeles Bejar alisema mgomo wake utadumu "mpaka suluhu ipatikane kwa uwindaji wa kinyama unaofanywa dhidi ya mwanawe'' / Picha : Reuters

Kizaazaa kinachomzonga rais wa shirikisho la la Uhispania Luis Rubiales, amejifungia kanisani na kuapa kutokula wala kunywa hadi wanaomshambulia mwanawe waachane naye.

Angeles Bejar alisema mgomo wake utadumu "mpaka suluhu ipatikane kwa uwindaji wa kinyama unaofanywa dhidi ya mwanangu kwa kitu ambacho hakistahili", kulingana na shirika la habari la EFE.

Shirika hilo la EFE limeripoti kuwa, Bi Angeles, alisubiri padre alipoondoka katika kanisa la Divina Pastora, lililoko kusini mwa Uhispania wanakotokea familia hiyo, kisha akajifungia yeye na dada yake.

Alimwomba Hermoso kusema ukweli na "kushikikilia taarifa ile ya kwanza aliyotoa,'' EFE iliongeza.

Rubiales alisimamishwa kazi siku ya Jumamosi na FIFA kufuatia busu lake mdomoni mwa nyota wa timu ya taifa ya wanawake Jenni Hermoso, wakati wa hafla ya utoaji tuzo baada ya Uhispania kushinda kombe la dunia mjini Sydney.

"Mwanangu hawezi kumdhuru mtu yeyote," Angeles alisema.

"Hakuna unyanyasaji wa kijinsia kwa kuwa kuna ridhaa kwa pande zote mbili, kama picha zinavyothibitisha," Angeles aliiambia EFE huku akihoji "kwa nini wanamzulia ?" na "ni nini nia yao ?".

Rubiales, mwenye umri wa miaka 46, amekuwa akipinga busu hilo - ambalo limeshutumiwa kuwa halitakiwi na Hermoso, wachezaji wenzake na serikali ya Uhispania - akihoji kuwa ni makubaliano.

Reuters