Huko Beni, Joel Kavuya, kijana ambaye amechukua jukumu la kusimamia karibu vijana 204 kwa kuwafundisha mchezo wa kuteleza ili kupunguza msongo wa mawazo na uhalifu mijini.
"Umri wa wachezaji wa mchezo kuteleza unatofautiana kati ya miaka 8 na 25, changamoto yetu kubwa ni wazazi kutotukabidhi watoto wao kwa kuhofia kuwa mchezo huu ni hatari," alisema Joel Kavuya, wakati wa mahojiano na TRT Afrika.
Ingawa jiji la Beni lina takriban kilomita 20 tu za barabara za lami, vijana hawa wamedhamiria kuwakilisha Kongo Mashariki kote ulimwenguni - Kongo ya Mashariki sio vita tuu lakini pia kuna "maisha".
Kikundi hicho pia hutoa mashauriano ya kisaikolojia kwa vijana baada ya Skating. Tunapokuwa pamoja kwenye mchezo wa kuteleza, tunasahau shida zote za kifamilia, nia ya kutumia dawa za kulevya na kiwewe kutokana na vita.
Kundi la Dreams Team Rollers liliundwa mwaka wa 2017 baada ya mwanzilishi wake kusafiri hadi Nairobi, Kenya na kuona watoto wakiteleza na furaha sana.
"Niliona kuwa watoto hawa walikuwa na furaha na tabasamu... nikajisemea, tunahitaji mchezo huu ili kuwavutia watoto hawa wenye kiwewe karibu nasi," anaongeza Bw. Kavuya.
Vijana hawa wanaoteleza wanaonekana kama mashujaa katika sehemu ya mashariki ya Kongo. Magari kadhaa yanasimama wanapowaona vijana hawa mashujaa wakija na viatu vyao vya kubingiria na wengine kuwapigia makofi.
"Wanapopita, wajenga hali ya furaha kwa idadi ya watu – Nimesha wayi simama mara kadhaa na gari langu ili kuwapa njia," alisema Jackson Kambale, dereva kutoka Beni.
"Hao ni mabalozi wetu…wote wana omba msaada toka kwetu" anaongeza Bw. Kambale