Katika mechi ya awali kati ya pande mbili siku ya Jumatatu, Uganda ilishinda Nigeria kwa wiketi tano. Picha:  Shirikisho la Kriketi la Nigeria /Twitter

Nigeria na wenyeji Rwanda watachuana kutinga fainali ya mashindano ya kriketi ya wanawake maarufu kama Kwibuka Womens T20 yanayoendelea Kigali, Rwanda siku ya Ijumaa.

Yellow Greens ya Nigeria itamenyana na timu thabiti, Victoria Pearls ya Uganda, ambao wako juu kwenye ubao na wanao ongoza wakiwa na alama 14.

Katika mechi ya awali kati ya pande mbili siku ya Jumatatu, Uganda ilishinda Nigeria kwa wiketi tano.

Uganda tayari wamefanikiwa kutinga fainali baada ya kushinda mechi zao zote saba hadi sasa. Rwanda, kwa upande wao, itacheza na Botswana, ambayo pia iliishangaza Nigeria kwa mikwaju 23 siku ya Alhamisi.

Rwanda na Nigeria zote zinashikana shingo na pointi nane kila moja. Timu zote mbili zilipoteza mechi tatu na kushinda nne.

Fainali imepangwa kufanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa Kriketi wa Rwanda mjini Kigali.

TRT Afrika