Timu ya taifa ya Soka ya Tanzania maarufu Taifa Stars itacheza mechi ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Niger na Morocco.

Wachezaji wa Timu ya taifa ya Soka ya Tanzania maarufu 'Taifa Stars' wameanza mazoezi baada ya kuripoti kambini kwa mazoezi ya siku saba.

Taifa stars itashuka dimbani Stade de Marrakech, nchini Morocco, Jumamosi ijayo Novemba 18 kuchuana na Niger kwenye kipute cha kufuzu Kombe la Dunia 2026.

Tanzania, imejumuishwa kundi E pamoja na Morocco, Niger, Congo na Zambia, kwa mechi za kufuzu kwa kombe hilo

Maandalizi ya timu hiyo yamepigwa jeki na rais wa Tanzania Samia Suluhu baada ya kuipa timu hiyo ndege ya kuisafirisha kuelekea Marrakech, nchini Morocco na kufupisha safari ya kikosi hicho kutoka Dar es Salaam hadi Marrakech.

Kikosi kamili cha wachezaji walioitwa kambini:

Magolikipa

Beno Kakolanya (Singida BS), Aishi Manula (Simba SC), Aboutwalb Mshery (Young Africans), Kwesi Kawawa (Karlslunden, Sweden), Metacha Mnata (Young Africans).

Mabeki

Dickson Job (Young Africans) Bakari Mwamnyeto (Young Africans) Ibrahim Hamad (Young Africans), Lusajo Mwaikenda (Azam FC), Nickson Kibabage (Young Africans), Haji Mnoga (Aldershot Town, Uingereza), Abdi Banda (Richards Bay, Afrika Kusini), Edward Manyama (Azam FC), Novatus Miroshi (Shakhtar Donetsk, Ukraine), Edwin Balua (Tanzania Prisons), Abdulmalik Zakaria (Namungo FC), Omar Mvungi (FC Nantes, Ufaransa).

Viungo

Ibrahim Joshua (Tusker FC, Kenya), Mzamiru Yassin (Simba SC), Sospeter Bajana (Azam FC) Baraka Majogoro (Chippa United, Afrika Kusini) Feisal Salum (Azam FC) Mudathir Yahya (Young Africans), Morice Abraham (FK Spartak, Serbia), Himid Mao (Tala'ea El Gaish, Misri), Ladaki Chasambi (Mtibwa Sugar)

Washambuliaji

Mbwana Samatta (PAOK FC, Ugiriki), Saimon Msuva (JS Kabylie, Algeria), John Bocco (Simba SC), Kibu Denis (Simba SC), Abdul Suleiman (Azam FC), Ben Starkie (Basford United, Uingereza) Matteo Anthony (Mtibwa Sugar), Charles M'mombwa (Macarthur, Australia) Clement Mzize (Young Africans).

TRT Afrika