Wachezaji wa Afrika Kusini wanasema wamejitolea kucheza Kombe la Dunia la Wanawake kufuatia kutatuliwa mizozo kuhusu malipo ya wachezaji na wafanyikazi wa usaidizi.
Mechi hiyo ya Jumapili 22 inatazamiwa kuwasha moto uwnajani wakati Uswidi inatafuta kwa udi n auvumba kuvunja mkosi wa miaka 32, angalau kujitafutia ubingwa wa dunia tena.
Lakini kibarua chao kigumu kwani Afrika Kuisni, ambao ndio mabingwa watetezi wa kombe la Afrika la wanawake WAFCON wamewachongea meno tayari kujisafisha sura, baada ya kufedheheshwa bila kushinda hata mechi moja walipoingia mara ya kwanza kombe la dunia 2019.
Banyana Banyana kwa takwimu
Banyanabanyana walibanduliwa kombe hilo katika awamu ya makundi kwa kucharazwa na vigogo Ujerumani, Uhispania na Chinam wanao orodheshwa na FIFA katika nafasi za 2, 6 na 14 bora duniani.
Afrika Kusini inashikilia nafasi ya 54 katika orodha hiyo.
Sweden ni mojawapo ya mataifa saba pekee yaliyoshiriki katika kila toleo la Kombe la Dunia la FIFA la Wanawake na hawajafungwa na timu yoyote ya Afrika katika mechi nne za mwisho za kombe la dunia.
Banyana hata hivyo wanajitosa uwanjani wakiju amacho yote juu yao baada ya zahma waliosababisha wakati wamaandalizi wa kombe hili na mechi za kirafiki, waliposusia mechi kadhaa kulalamikia haki ya marupurupu na mengine.
Jumamosi, nahodha Refiloe Jane alithibitisha kwamba mizozo yote na shirikisho la Afrika Kusini ilikuwa imesuluhishwa kabla ya kuanza kwa mashindano, ikiwa ni pamoja na kuhakikishiwa malipo ya $ 30,000 kwa kila mchezaji ambayo hapo awali iliahidiwa na FIFA.
"Tulikuja New Zealand tukiwa tumetatua shida zetu zote. Na tulipoondoka Afrika Kusini, tulilihakikishia taifa kuwa kila kitu kimekuwa sawa. Kwa hivyo kuja katika mashindano haya umakini wetu umekuwa tu kuangazia mpira wa miguu.