Wanariadha wa Kenya walitawala katika mkondo wa mwisho wa mzunguko wa Diamond League mjini Brussels Jumamosi usiku huku Faith Cherotich, Faith Kipyegon, Beatrice Chebet na Emmanuel Wanyonyi wakishinda katika mbio zao.
Cherotich aliwapa watu shoo kubwa kwa kujinyakulia ushindi wake wa kwanza wa Diamond League alipotumia 9:02.36 kushinda mbio za wanawake kuruka viunzi.
Wilfred Yavi, Mkenya anayekimbilia Bahrain alilazimika kuchukua nafasi ya pili aliposhindwa kumudu hali ya hewa ya Brussels na upepo mkali alioachiwa nyuma na Faith Cherotich na kumaliza kwa muda wa 9:02:87 huku Mganda Peruth Chemtai akiishia katika nafasi ya tatu kwa kwa 9:07.60.
"Sikutarajia kushinda leo, lakini nadhani nilikimbia mbio nzuri. Haikuwa rahisi, lakini niliendelea kujiambia kwamba, ikiwa bado niko katika uongozi baada ya kuruka maji mara ya mwisho, ningeshinda. Kushinda Ligi ya Diamond kunamaanisha mengi kwangu,” Cherutish alisema.
'Little Faith' kama anavyofahamika zaidi - amekuwa mara kwa mara kwenye jukwaa la hafla za Ligi ya Diamond mnamo 2024, pamoja na Xiamen (wa pili), Prefontaine (wa 3) na Roma (wa 3).
Wakati huo huo, Mkenya mwingine Faith Kipyegon aliongezea dhahabu yake ya Diamond League alipoweka rekodi ya 3:54.75 na kushinda mbio za mita 1500 kwa wanawake.
Diribe Welteji wa Ethiopia alimaliza wa pili kwa 3:55.25 huku Jessica Hull wa Australia akikamilisha nafasi ya mwisho ya jukwaa baada ya kutumia 3:56.99.
Bingwa wa rekodi ya dunia ya mbio za mita 10,000 kwa wanawake, Beatrice Chebet, alihitimisha msimu wake bora kwa ushindi katika mbio za 5000m.
Bingwa huyo wa Olimpiki wa mita 5000 na 10,000 alifikisha rekodi ya saa 14:09.82 na kuvuka mstari wa mwisho mbele ya Medina Eisa (14:21.89) na Fotyen Tesfaye (14:28.53), wote wa Ethiopia, waliomaliza wa pili na wa tatu mtawalia.
Ushindi wa Chebet katika mji mkuu wa Ubelgiji ulikuwa wa nne katika kampeni ya mwaka huu ya Diamond League baada ya kushinda huko Doha (m 5000), Prefontaine Classic (m 10,000), na Zurich (m 5000).
Usiku haungeisha vyema zaidi kuliko onyesho lingine la kutisha kutoka kwa Emmanuel Wanyonyi ambaye aliibuka na ushindi katika mbio za mita 800 za wanaume.
Bingwa huyo wa Olimpiki wa mita 800 alitumia muda wa 1:42.70, mbele ya Mualgeria Djamel Sedjati (1:42.86) na Mkanada Marco Arop (1:43.25) katika nafasi ya pili na ya tatu mtawalia.
Ushindi wa mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 20 ulikuwa wa kuridhisha zaidi na kuli[piza kisasi baada ya kukatishwa tamaa katika mkondo wa mwisho wa mzunguko huko Silesia ambapo alitolewa rangi na Mkanada huyo katika kumaliza.
Huku rekodi ya dunia ya David Rudisha ya 1:40.91 ingali imesimama, ushindani kati ya watatu - pamoja na Mfaransa Gabrial Tual - 2025 utakuwa mwaka wa kuvutia kutazamiwa kwa upande wa 800m ya wanaume.