Mkenya Faith Kipyegon amekuwa mwanamke wa kwanza kukamilisha mbio za mita 1,500 na mita 5,000 kwenye Mashindano ya Dunia baada ya kushinda mbio za masafa marefu ndefu siku ya Jumamosi.
Siku nne baada ya kushinda mbio za mita 1,500, mshindi huyo wa medali ya dhahabu mara mbili katika Olimpiki alimvuka Mholanzi Sifan Hassan katika lala salama na kuvuka dakika 14 sekunde 53.88 kwa fainali nyingine nzuri.
Dhahabu mbili za Kipyegon kutoka Budapest ni msimu wa ajabu ambapo alivunja rekodi tatu za dunia - katika mbio za mita 1,500, maili na 5,000.
"Huu umekuwa mwaka wa kustaajabisha kwangu. Kuweka historia leo, kushinda medali mbili za dhahabu katika michuano ndio nilikuwa nikiota msimu huu," mchezaji huyo wa miaka 29 alisema.
"Nimekuwa mvumilivu nikisubiri niweze kuvunja rekodi za dunia na kushinda dhahabu mara mbili.... Lakini ndoto yangu imetimia, inashangaza. Nimekuwa nikijisukuma zaidi ya uwezo wangu na nitaendelea kujitutumua mbeleni.
kwa upande wake Siffan Hassan, mshindi wa medali ya shaba katika mbio za 1,500, alipanda daraja hadi fedha kwa 14:54.11. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 30 alistahimili changamoto kubwa mara tatu huko Budapest, akianza mashindano hayo kwa kuanguka mita 20 tu kutoka kwenye mstari wa kumaliza katika mbio za mita 10,000.
"Michuano hii imenifundisha mengi. Imenipa ujasiri zaidi kwa sababu nilihamia marathon mwaka huu na kwa miaka miwili sijafanya kazi yoyote ya kasi," alisema Hassan, ambaye alishinda marathon ya London mnamo Aprili, yake ya kwanza kwa umbali huo.
"Jinsi nilivyoweza kukimbia mwishoni sijui. Nilihisi ajabu kwenye mzunguko wa mwisho na ilikuwa tu katika mita 20 za mwisho sikuweza kushikilia. Faith alikuwa na nguvu kuniliko mimi leo."