Shirikisho la soka la Afrika (“CAF”) lilitangaza Tuzo la Pesa kwa Uzinduzi wa shindano la Ligi ya Soka ya Afrika (“AFL”) ambalo litashirikisha Vilabu vya soka vilivyo na viwango vya juu na vilivyo na mafanikio zaidi katika Bara la Afrika.
Miongoni mwa zawadi nono ni Dola milioni nne za Marekani kwa mshindi wa ligi hiyo na kwa kuwa hakuna duru za awali kabla ya robo fainali, ina maana waliofuzu kucheza, vilabu vinane vyote vinaingia moja kwa moja kwa robo fainali, na pia wanapokea kila klabu dola milioni moja kwa kushiriki robo fainali.
- $4,000,000 kwa Mshindi
- $3 000 000 kwa Mshindi wa Pili
- $1 700 000 kwa kila waliofuzu Nusu fainali
- $1 000 000 kwa kila mmoja wa Robo-fainali
AFL itaanza Ijumaa tarehe 20 Oktoba 2023 jijini Dar es Salaam, Tanzania kwa mechi ya ufunguzi kati ya Simba SC (Tanzania) na Al Ahly SC (Misri).
Ligi hiyo inaanza mwaka mmoja tangu izinduliwe na Shirikisho la Soka Afrika CAF.
AFL ni shindano la CAF lililoanzishwa kwa ushirikiano na FIFA. Mojawapo ya malengo makuu ya kuunda AFL ni kuhakikisha kwamba ubora wa kandanda ya Vilabu vya Afrika unashindana kimataifa na Vilabu vya Soka vya Kiafrika vinajiendesha kibiashara.
CAF inasema kuwa AFL pia itachangia katika ukuzaji na ukuzaji wa vipaji vya kandanda ya Vijana katika Bara la Afrika.
''Nia ya CAF, ni kwamba mashirika yote ya soka kutoka nchi wanachama 54 ikiwa ni pamoja na nchi ambazo huenda hazina Vilabu vya soka katika AFL zifaidike na kupokea michango ya kifedha kutokana na uwezekano wa kibiashara na mafanikio ya AFL.
Vilabu vingine maarufu na vya juu zaidi vya kandanda vinavyoshiriki ligi hii ya Uzinduzi wa AFL ni Enyimba FC (Nigeria), Wydad AC (Morocco), Mamelodi Sundowns FC (Afrika Kusini), TP Mazembe (DR Congo), Espérance Sportive de Tunis (Tunisia) na Atlético Petróleos de Luanda (Angola).
Mfumo utakaotumika katika ligi ya AFL
Timu zilizochaguliwa zitacheza katika mfumo wa mtoano unaojumuisha robofainali, nusu fainali na fainali.
Mechi zitachezwa kwa awamu mbili, mechi ya nyumbani na ugenini na sheria ya FIFA ya bao la Ugenini itatumika.
Ikitokea sare baada ya kumalizika kwa mkondo wa pili, hakutakuwa na muda wa ziada katika hatua ya robo fainali au nusu fainali, mechi itaenda moja kwa moja kwa mikwaju ya penalti.
VAR itatumika kwa kila mechi katika Ligi ya Soka ya Afrika.