Meneja wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger ameomba msaada kwaajili ya waathiriwa wa matetemeko makubwa ya ardhi yaliyotikisa kusini mwa Uturuki na sehemu za Syria mnamo mwezi Februari.
"Watu wa Uturuki wanahitaji msaada wako katika wakati huu mgumu sana," Wegner alisema katika video iliyotolewa Ijumaa na Shirikisho la Soka la Uturuki (TFF). "Tunakualika usaidie, ikiwa unaweza."
Kampeni ya misaada ya Bega kwa Bega kukusanya michango kwa ajili ya wahanga wa tetemeko hilo itaendelea hadi Juni 15 chini ya uongozi wa Wizara ya Vijana na Michezo ya Uturuki, TFF, Super League Clubs Association Foundation na beIN Media Group.
Matetemeko ya ardhi ya 7.7- na 7.6 katika kipimo cha Richter yalipiga mikoa 11 ya Uturuki Februari 6 -- Adana, Adiyaman, Diyarbakir, Elazig, Hatay, Gaziantep, Kahramanmaras, Kilis, Malatya, Osmaniye na Sanliurfa.
Zaidi ya watu 50,000 huko Uturuki walikufa kutokana na matetemeko ya ardhi yaliyo athiri watu milioni 13.5 nchini humo, pamoja na wengine wengi kaskazini mwa Syria.
Wenger, 73, alitwaa Vikombe saba vya FA vya Uingereza na mataji matatu ya Ligi Kuu ya Uingereza, moja wakati akiwa na The Gunners kuanzia 1996 - 2018.