Gambia wako na nafasi nzuri ya kupenya kwani wanahitaji japo alama moja tu / Photo: AFP

Kocha wa Ufaransa Landry Chauvin ameonesha kuwa na imani na vijana wake licha ya kichapo walichopata kutoka kwa Jamhuri ya Korea.

Vijana hao walipozungumza baada ya mechi, walielezea kuhuzunishwa na matokeo japo kocha Chauvin ana amini bado wanaweza kujikwamua katika mechi yao ya pili.

Ushindi au droo inawatosha Gambia kuingia robo fainali huku Ufaransa wakiwa na dharura ya kushida kwani wanaingia uwanjani bila alama, kwa hiyo ushindi pekee ndio utakao wakomboa.

Naye Kocha wa Gambia amenukuliwa katika mtandao wa twitter wa Gam Football, kuwa ananuia kufanyia mabadiliko jeshi lake. “Tunaweza fanya mabadiliko kadhaa, kwani ukitazama mechi zilizotangulia, tulipata matokeo mazuri tulipowaleta wachezaji wetu wa ziada.‘’

Tunisia wanalazimika kushinda mechi yao Alhamisi au wakabiliwe na kubanduliwa : Picha AFP

Tunisia pia wanatetereka wanapoingia uwanjani wakiwa na pigo kutoka mechi yao ya awali waliokutana na England.

Hata hivyo wachambuzi wanatazama wapinzani wao wa Alhamisi Iraq, kuwa wepesi kuliko England.

Tunisia wananuia kuwapa Iraq pigo kama walichokipata kutoka kwa Uruguay waliowapa 4-0.

TRT Afrika