Hii itakuwa mechi ya kwanza kati ya Tanzania na DR Congo katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika. / Picha : TRt Afrika

Hatua ya makundi ya AFCON 2023 inafikia tamati siku ya Jumatano.

Karata zote leo uwanjani Taifa Stars wanapotibuana na Chui wa Congo katika mechi yao ya tatu na mwisho ya kundi F, huku timu tatu kati ya nne zikiwa bado na nafasi ya kumaliza juu ya jedwali, na timu zote nne zina fursa ya kufuzu kwa raundi ya muondoano katika nafasi ya pili. Bidii ni yao tu.

Tanzania hata hivyo ndio wanaokabiliwa na kibarua kigumu zaidi , kuelekea katika mechi mkiani mwa kundi lao ikiwa imechukua pointi moja pekee kutoka kwa mechi mbili za kwanza.

Wakishinda mechi yao ya Jumatano, Itakuwa ushindi wa kwanza kabisa kwenye michuano yoyote ya AFCON na utawawezesha kuruka jedwali na kupenya kundini. Wametoka sare mbili na kupoteza mechi sita kati ya nane za AFCON kufikia hatua hii.

Hii itakuwa mechi ya kwanza kati ya Tanzania na DR Congo katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika./ Picha : TRT Afrika 

Hata hivyo, walionekana kushika usukani katika mchezo wao wa mwisho - sare ya 1-1 na Zambia - ambayo ilikuwa ni mara ya tatu tu kuwahi kuongoza katik amechi yoyote ya Afcon. Zaidi ya hayo, mara nyingine mbili zote zilikuja katika mchezo mmoja, na wakaishia kupoteza mechi hiyo - kichapo cha 3-2 kutoka kwa Kenya katika toleo la 2019.

Kwa upande wake DR Congo wametoka sare katika michezo yao yote miwili katika AFCON 2023 na kukaa sawa na Zambia katika Kundi F wakiwa na rekodi sawa. Ikiwa Morocco itaifunga Zambia katika mechi nyingine ya kundi hilo, DR Congo itahitaji pointi moja tu dhidi ya Tanzania ili kuthibitisha nafasi ya pili.

Takwimu zao

Hii itakuwa mechi ya kwanza kati ya Tanzania na DR Congo katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika.

Tanzania na DR Congo zilikutana mara ya mwisho Novemba 2021 - DR Congo ilishinda 3-0 jijini Dar es Salaam katika mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia la FIFA.

Tanzania imesalia bila ushindi kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika, ikicheza mechi nane bila mafanikio (D2 L6), ingawa ilifanikiwa kuepuka kushindwa katika mechi yao ya mwisho, ikitoka sare ya 1-1 na Zambia.

DR Congo wametoka sare katika mechi zao zote mbili za AFCON 2023 - mara ya mwisho kutoka sare katika mechi zote tatu za hatua ya makundi kwenye AFCON ilikuwa 2015, na kumaliza katika nafasi ya tatu kwa jumla katika michuano hiyo.

DR Congo wameshinda mechi nne pekee kati ya 22 zilizopita kwenye AFCON ingawa hawajafungwa katika mechi zao nne zilizopita.

TRT Afrika