Na Salman Niyazi
Mazungumzo kuhusu mustakabali wa vikwazo dhidi ya Syria yanaendelea ndani ya kumbi za mikutano mjini Brussels.
Haya ndiyo mabadiliko yanayoendelea kujitokeza baada ya kuanguka kwa utawala wa Bashar al-Assad mwezi Disemba mwaka 2024.
Historia ya vikwazo dhidi ya Syria inarudi nyuma mpaka mwaka 2011, wakati utawala dhalimu wa Assad ulipositisha ushirikiano na nchi za Jumuiya ya Ulaya.
Vikwazo hivyo viliathiri biashara kwa kiasi kikubwa huku taasisi za kifedha za Syria zikipigwa marufuku kufungua matawi ndani ya Umoja wa Ulaya.
Kwa sasa, Jumuiya ya Ulaya iko katika jitihada za kupitia upya vikwazo hivyo.
"Tutaamua kusitisha baadhi ya vikwazo kwenye sekta ya nishati na usafiri," amesema Waziri wa Mambo ya Nje Jean-Noël Barrault.
Hata hivyo bado Jumuiya ya Ulaya inaweka masharti magumu ikiwemo kuitaka Syria ipambane na magaidi wa DAESH.
Mwezi Disemba, Rais wa Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen, alionya kuwa mabadiliko ya uongozi ni fursa yenye matatizo.
Syria imekuwa ikipokea misaada mikubwa kutoka Umoja wa Ulaya, yenye kufikia Dola Bilioni 35.
Hata wakati wa vikwazo, Umoja wa Ulaya uliendelea na misaada hiyo.
Hata wakati wa vikwazo, Umoja wa Ulaya uliendelea na misaada hiyo.
Uchumi dhoofu
"Bila maendeleo ya kiuchumi, tunaweza kurudi kule kule," – maneno ya Ahmed al-Sharaa yanatafsiriwa kama hukumu.
Kiongozi huyo mpya wa Syria hajatia chumvi yoyote. Huduma umeme inapatikana kwa saa moja tu kila siku huku kukiwa na uhaba mkubwa wa fedha.
Syria inakabiliana na mfumuko mkubwa wa bei na ukosefu mkubwa wa ajira.
Utawala mpya wa Syria una njia mbili kwa sasa.
Ya kwanza ni kupambana na DAESH nay a pili ni ya kuishirikisha Urusi ambayo inataka kuweka kambi za kijeshi katika maeneo ya Tartus na Khmeimim kwa ahadi ya kuisaidia Syria kiuchumi.
Ukiwa umerithi deni la Dola Bilioni kutoka Urusi, utawala mpya wa Syria utakuwa unatafakari namna ya kutumia vizuri fursa hiyo. "Hakuna maadui wa kudumu katika siasa," anasema Waziri wa Ulinzi wa Syria Murhaf Abu Qasra.
Wakati huo huo, uchumi wa nchi hiyo unazidi kudorora.
Mwezi mmoja baada ya kuangushwa kwa utawala wa Assad, mwakilishi wa Rais wa Urusi Mikhail Bogdanov aliwasili Damascus kwa ajili ya majadiliano.
Hii ilifuatiwa na mazungumzo ya njia ya simu kati ya Vladimir Putin na Ahmad al-Sharaa yaliyofanyika Februari 12.
"Suala la msingi kwa sasa ni hofu ya kuona kilichotokea Libya kinatokea kwa Syria," alibainisha Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi.
Kulingana na Bloomberg, Urusi inakaribia kukamilisha mazungumzo na utawala mpya wa Syria.
Kwa upande wake, Syria iko tayari kwa makubaliano na Urusi, madhali yatanufaisha nchi hiyo.
Urusi pia iko tayari kufanikisha ujenzi wa Syria, ikiwemo kuipa misaada ya kijeshi.
Kwa upande mwingine, Umoja wa Ulaya unahofu juu ya mkakati wa Urusi, ukisema kuwa utahatarisha usalama wa Ulaya.