Kushindwa kwa vyombo vya habari vya kimataifa kuangazia mapigano yanayoendelea nchini Sudan ni suala linalogonga vichwa vya wengi kwa sasa./Picha: AFP    

Na Abdalftah Hamed Ali na Sarah Khamis

Toka kuibuka kwa vita hivyo mwezi Aprili 2023, taifa la Sudan limekuwa katika hali mbaya ya kisiasa, kiuchumi na kibinadamu.

Licha ya ukubwa wa janga hilo, bado ulimwengu unaendelea kufumbia macho tatizo hilo tofauti na inavyofanya kwa machafuko ya Mashariki ya Kati, ikiwemo Gaza, Lebanon, na yale ya hivi karibuni huko Syria.

Janga hilo limewaacha zaidi ya watu milioni 30 nchini humo wakiwa katika ukame mkubwa hasa katika eneo la Darfur Kaskazini, iliyopo kambi ya wakimbizi ya Zamzam./Picha: AFP

Inashangaza kuona janga hilo kuendelea kufumbiwa macho na vyombo vya habari vya kimataifa.

Janga kubwa la kibinadamu

Zaidi ya watu milioni 14, ambayo ni sawa ya asilimia 30 ya idadi ya watu wa nchi hiyo wamekosa makazi toka mwezi Agosti 2023, huku wengine milioni 11 wakigeuka kuwa wakimbizi wa ndani , kulingana na utafiti wa hivi karibuni uliuofanywa na shirika la Umoja wa Mataifa.

Cha kushtua zaidi ni kuwa zaidi ya asilimia 53 ya wakimbizi wa ndani ni watoto walio chini ya miaka 18. Janga hilo limewaacha zaidi ya watu milioni 30 nchini humo wakiwa katika ukame mkubwa hasa katika eneo la Darfur Kaskazini, iliyopo kambi ya wakimbizi ya Zamzam.

Kulingana na UNICEF, watoto wengi watakabiliwa na utapiamlo mwaka huu, kutokana na machafuko ya kisiasa nchini humo./AFP

Takwimu hizi si za kufikirika, bali zinatokana na uhalisia wa mauaji na mateso ya raia wa Sudan unaosababishwa na kufikiwa makubaliano ya kuweka silaha chini.

Kikundi cha wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF) –kilichoanzishwa na serikali ya nchi hiyo, kwa kiasi kikubwa kilihusika na matukio ya ubakaji, mauaji ya kimbari na ya kikabila.

Mwanzoni mwa mwezi Disemva 2024, watu wapatao 127, wengi wakiwa ni raia waliuwawa ndani ya siku mbili, kwa mujibu wa wanaharakati wa haki za kibinadamu. Mashambulizi hayo ni sehemu ya mpango unaowalenga jamii za watu wa Masalit, ambapo kulingana na jumuiya ya kimataifa, kosa hilo ni ukiukwaji wa haki dhidi ya utu.

Huku hayo yakiendelea, njaa pia imetumika kama kigezo cha kuendeleza mapigano hayo./Picha: Reuters

Huku hayo yakiendelea, njaa pia imetumika kama kigezo cha kuendeleza mapigano hayo.

Wanamgambo wa RSF wanashutumiwa kutumia uwepo wa njaa kama kisingizio cha kuendeleza mapigano hayo.

Kusudio la RSF ni kuona kuzuia misaada ya kibindamu kuwafikia walengwa, hasa katika maeneo ya Zamzam.

Kulingana na UNICEF, watoto wengi watakabiliwa na utapiamlo mwaka huu, kutokana na machafuko ya kisiasa nchini humo.

Kwa mfano, katika kambi ya wakimbizi ya Zamzam, robo ya watoto waliofanyiwa uchunguzi walibainika kuwa na utapiamlo uliokithiri, kulingana na Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka.

Licha ya hali hiyo, machafuko ya nchini Sudan hajayaangaziwa vya kutosha.

Vita vya Sudan si ni janga la taifa tu, bali hali yenye kuvuruga eneo lote la Pembe ya Afrika. Wakimbizi wanaokimbia machafuko hayo kwa sasa wanaelekea Chad, Misri, na Sudan Kusini, mataifa ambayo pia yanakabiliwa na changamoto mbalimbali.

Hata njia muhimu za kibiashara za kuelekea Afrika Mashariki na El Gezira zimeathirika kutokana na machafuko hayo, huku wanamgambo wa RSF wakionesha kuzidiwa baada ya makamanda wake kulikimbia kundi hilo.

Vita vya Sudan si ni janga la taifa tu, bali hali yenye kuvuruga eneo lote la Pembe ya Afrika./Picha: AFP

Kwa upande wake, jeshi la Sudan limeendelea mapambano kwa nia ya kutwaa maeneo mbalimbali katika jiji la Khartoum na majimbo ya Sinar.

Hata hivyo, licha ya uhalisia huu, bado machafuko ya nchini Sudan hayajaangaziwa vya kutosha na jumuiya na vyombo vya habari vya kimataifa.

Wakati vyombo hivyo vikitupia vita vya Ukraine na vile vya Gaza, hata kuelekea Lebanon na kuanguka kwa utawala wa Assad nchini Syria, hali ni tofauti kwa Sudan.

Kimsingi, wanahabari hawapewi nafasi ya kuangazia yale yanayoendelea nchini Sudan huku wengi wakilazimika kuikimbia nchi yao kwa hofu ya usalama.

Hali hii inawakumba pia waandishi wa nje ambao pia wanashindwa kuingia nchini humo.

Kwa sasa, ni kama hakuna anayejali na kinachoendelea nchini Sudan.

Mbaya zaidi, hata kampeni za kupinga vita hivyo hazipati fedha za kutosha kuwawezesha kuendesha shughuli zao.

Kufikia sasa, ni asilimia 32 ya Dola Bilioni 2.7 kutoka za Umoja wa Mataifa zimeweza kutolewa, huku taasisi za misaada zikisisitiza haja na umuhimu wa kuunga mkono vikundi vinavyojitoa kwenye vita hivyo.

Vyombo vya habari vya kimataifa vina jukumu muhimu katika kukuza sauti za waathirika wa Sudan na kuwawajibisha wahalifu kwa vitendo vyao vya uhalifu.

Kwa kupaza sauti, vyombo vya habari vitaongeza shinikizo kwa serikali, mashirika yasiyo ya Kiserikali na taasisi za misaada.

Mbaya zaidi, hata kampeni za kupinga vita hivyo hazipati fedha za kutosha kuwawezesha kuendesha shughuli zao./Picha: AFP

Hali kadhalika, ni lazima kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua za makusudi kuingilia kati suala hilo.

Ni muhimu pia kuzipa nguvu taasisi zinazosimamia uwajibikaji ikiwemo Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kuhakikisha kuwa waathirika wa machafuko hayo wanapata haki na kwa wakati.

Hata kuchaguliwa kwa Donald Trump kama Rais wa Marekani unaweza ukaongeza changamoto zaidi.

Abdalfatah Hamed Ali ni mtaalamu wa masuala ya Mashariki ya Kati wakati Dkt Sahar Khamis ni mtaalamu wa vyombo vya habari cya Kiislamu na Kiarabu.

TRT Afrika