Zuchu ndiye mwimbaji pekee wa kike aliyeyachaguliwa kutoa burudani katika tamasha hilo.
Mitindo ya mashabiki kurusha vitu jukwaani kwa wasanii wengi zilizoshamiri siku za karibuni umeibua hisia za wengi nchini Tanzania baada ya nyota wa muziki, Zuhura Othman Soud, maarufu kwa jina la Zuchu, kuwa msanii wa hivi karibuni kupigwa wakati akitumbuiza.
Tabia hii ilifanya vichwa vya habari vya kimataifa kwa mara ya kwanza mwezi wa Juni, wakati mwimbaji na mtunzi wa nyimbo wa Uingereza Harry Styles alipopigwa jichoni na kitu kilichorushwa kutoka kwenye jukwaa alipokuwa akitumbuiza kwenye Uwanja wa Ernst Happel nchini Austria.
Ilifuatiwa haraka na mfululizo wa matukio ya kurusha vitu kwa watumbuizaji kama vile Bebe Rexha na Kelsea Ballerini, ambaye mshambuliaji wake alikamatwa.
Wote wawili walijeruhiwa katika mchakato huo, na walituma picha za macho yao yaliyojeruhiwa kwenye mitandao ya kijamii baada ya matukio hayo.
Katika tukio hili la hivi karibuni linalomhusisha Zuchu, kanda za video zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha mwimbaji huyo akiwa katikati ya msururu wa wanenguaji wake wakati kitu cha kuruka kilichorushwa kutoka kwa umati wa watu waliokuwa wakishangilia kilipomgonga machoni.
Tukio hilo lilitokea wakati Zuchu alipokuwa akitumbuiza kwenye tamasha la awali la Wasafi Festival Ijumaa kabla ya tamasha kuu Jumamosi.
Zuchu mara moja alionekana kupepesuka na kupatwa kwa maumivu na kuyafunika macho yake kwa mikono miwili kabla ya kutolewa haraka na kutoka jukwaani. Kisa hicho kilimlazimu Zuchu kukatisha kutoa burudani.
Msanii huyo bado hajazungumzia tukio hilo hadharani na haikufahamika mara moja iwapo alijeruhiwa.
Mwimbaji huyo ambaye amesainiwa na lebo ya rekodi ya Diamond Platnumz ya WCB, ndiye mwimbaji pekee wa kike aliyechaguliwa kushiriki katika tamasha hilo la Wasafi Festival 2023.