Diamond anaongoza kwa wimbo nambari mbili za kwanza katika views nchini Tanzania / Picha : X- Simba 

1. Yatapita Diamond Platnumz (Views milioni 37)

Kibao cha kwanza kilichopepea zaidi YouTube kwa 'views' ni ngoma ya Yatapita, huku ngoma huiyo ikiwa ndio kama 'kurejea rasmi' jukwaani Kwa Simba, Diamond Platnumz kwenye muziki wa Bongo Fleva. Wimbo huo unaonekana kupokelewa vyema na mashabiki kwani video hiyo ilijizolea views Milioni 10 chini ya muda wa mwezi mmoja.

2. Zuwena - Diamond Platnumz (views milioni 24)

Diamond Platnumz alizidi kutawala anga za YouTube Afrika Mashariki huku wimbo wake wa 'Zuwena' ukiibuka katika nafasi ya pili kwenye jedwali la views. Usimulizi na hisia zilizoko kwenye video hiyo iliyosimuliwa kwa ubunifu wa hali ya juu, ulidhihirisha kwa nini ilipokea ushabiki wa kiwango hicho.

3. Single Tena-Harmonize (Views Milioni 20)

Konde boy, Harmonize naye amejidumisha kwenye steji licha ya kukata uhusiano na wasafi huku akionyesha ubabe wake kwenye muziki. Mchanganyiko wake wa Bongo Fleva na Amapiano umemfanya ajidumishe jukwanni.

4. Mahaba - Ali Kiba (Views Milioni 16)

King Kiba, Ali Kiba, anashikilia nafasi ya tatu huku nyota huyo, aliyevuma na ngoma ya 'mnyama' kwa ajili ya klabu ya Simba, amepokea sifa na mahaba nyingi kwa ajili ya 'Mahaba' ambayo ilitumia eneo moja tu tangu mwanzo hadi mwisho kwenye video. Video hiyo ni rahisi yaani simple sana lakini yenye maelezo mengi, na kama kawaida ilionyesha hisia za Ali Kiba na utendaji wake mzuri wakati wote.

5. Zuchu - Utaniua

Nafasi ya tano imechukuliwa na wimbo wa Zuchu wa 'Utaniua' uliomshirikisha Diamond Platnumz. Ufanisi wa video hiyo ulionekana 'pap' mara moja tu ndani ya saa chache baada ya kudondoshwa. Aidha, Utaniua ni video ya Muziki ya Zuchu iliyotazamwa zaidi ndani ya 2023.

TRT Afrika