Na Jacob Katumusime
Wakongwe wanasema, jina la Makerere lilianza tangu karne ya 18 enzi za Mfalme Kabaka Ssemakokiro ambae alikuwa akiamka asubuhi mapema katika kasri yake iliyokuwa mlimani kilipo Chuo Kikuu ili kuupata muonekano mzuri wa Ziwa Nalubaale linaloonekana kwa mbali.
Kwa lugha ya kiganda, mshangao aliokuwa nao Kabaka pindi anapoona uzuri wa ziwa asubuhi mara nyingi ulikuwa ni, ‘Kabaka ayagala kulaba mazzi makereere!’ Mfalme alipohamisha kasri yake, mlima ulifufua mvuto wake na kuitwa Makereere. Vyovyote itakavyokuwa, funzo lililopo hapa ni kwamba, kila mtu sharti aamke mapema ili apate akitakacho.
Tangu kuasisiwa kwake, Chuo Kikuu cha Makerere kimekuwa kikirauka
Hivi karibuni, katika kuadhimisha miaka 100 ya kuasisiwa, Makerere inakumbuka baada ya zaidi ya miongo miwili ya kuanzishwa, ilivyoruhusu kundi la kwanza la wanafunzi wa kike kujiunga na chuo, na hatimae kubadilisha kauli mbiu yake, kutoka, `Wacha Tuwe Wanaume` na kuwa ‘Tunajenga kwa Ajili ya Maisha ya Baadae.`
Katika miongo iliyofuata, Makereere ilikuwa inasajii wanafunzi watakaobadilisha muonekano wa ulimwengu unaowazunguka.
Mbali na kuzalisha wataalamu wenye ueledi wa kiwango cha juu, Makerere pia imetoa zaidi ya marais watano baada ya ukoloni wakiwemo Mwalimu Julius K. Nyerere, Apollo Milton Obote, Benjamin Mkapa, Paul Kagame, Mwai Kibaki, na Joseph Kabila.
Kizazi cha Makerere kimeandika historia ya ushindi na majanga
Makerere, kama mzazi yoyote alivyo, inafurahia watoto wake wote.
Fahari ya vizazi vya waliotoka Makerere sio tu kwa wale waliohitimu lakini kama Chuo Kikuu kinavyonadi katika wimbo wake wa chuo, kwamba, na wote `Waliopita katika langu kuu la Marekere.`
Ushawishi mkubwa wa kizazi kilichotoka katika Chuo hicho ni baada ya uhuru ambapo palikuwa ndio kitovu cha wanafalsafa.
Mnamo mwaka 1961, Rajat Neogy alianzisha jarida la `Transition` chuoni hapo.
jarida hilo lilikuwa ni uwanja wa vita wa fikra ambao wasomi na wanasiasa nguli walipikwa.
Jarida lilivutia sauti muhimu ndani na nje ya bara la Afrika ikiwemo washindi wa Tuzo ya Nobel Martin Luther King Jr, Nadine Gordimer na Wole Soyinka.
Bessie Head, Langstone Hughes na James Baldwin pia walikuwa wachangiaji wakubwa katika jarida hilo.
Haishangazi, kuona kwamba, Makerere ilikuwa mwenyeji mwa kongamano la kihistoria la waandishi wa kiafrika kwa lugha ya kiengereza mwaka 1962.
Kongamano hilo, liliwakutanisha wanafasihi nguli na chipukizi chini ya paa moja.
Hapo ndipo Chinua Achebe alipokutana na James Ngugi, mwanafunzi ambae baadae alibadilisha jina na kujiita Ngugi wa Thiong’o.
Makerere imetilia mkazo sio tu katika mijadala bali pia imekuwa ni sehemu muhimu kwa wapigania uhuru.
Kwa mfano, rais Jomo Kenyatta wa Kenya aliyetunukiwa shahada ya heshima mwaka 1963 kwa ukombozi wa nchi yake. Uhusiano wake na Chuo Kikuu cha Makereere unaonyesha umuhimu wa Chuo hicho katika harakati za kujikomboa kwa bara la Afrika.
Makerere imekuwa fahari ya afrika
Mara kwa mara unasikia misemo kama vile ‘Makerere ndio chuo kikuu pekee kilichopo magharibi mwa bahari ya hindi, kusini mwa Sahara, kaskazini mwa Limpopo na mashariki mwa Congo.’
Wanafunzi waliomaliza wa Makerere mara nyingi hujigamba kwamba nchini uganda, Makerere bado ni mlima wenye kiwango kikubwa cha akili.
Kwa hakika, katika majina maarufu ya vyuo vikuu, jina la Makereere linajitosheleza, ukitaja ‘Makerere’ na kuongeza ‘Chuo Kikuu` ni kama kujirudia.
Je, Makerere imewezaje kuishi kwa uwezo wake na kubadiisha dunia ambayo tumeirishi hii leo?
Miaka yote ya 60, washirika wa Makerere, wasomi, wanafunzi waliohitimu na na ambao bado wamekua ni watu wasioshindwa. Okot p’Bitek alikatiza utamaduni wa fasihi ya kikoloni kwa machapisho yake makali ya sura za kiafrika, zijulikanazo kama Song of Lawino.
Ngugi wa Thiong’o na wenzie walianzisha vurugu katika vyuo vikuu vya kiafrika na kampeni kali ya kutaka kuondolewe kwa idara za kiengereza.
Wawili hao, p’Bitek na Ngugi baadae walijaribu kupeleka chuo kikuu kwa jamii kupitia matamasha ya mila na tamaduni na uingizaji wa hadharani nchini Kenya na Uganda.
Nchini Tanzania, kwa mfano, Nyerere alikuwa anajaribu kuondoa matabaka ya kikoloni na kujenga dira ya usawa miongoni mwa wananchi wake.
Wanafunzi wa Makerere walikuwa wakipanga kufanya maandamano dhidi ya ubaguzi wa rangi wa Afrika Kusini, dhidi ya Marekani, na maandamano ya kila aina dhidi ya mafashisti.
Hata hivyo, aliyekuwa mwanachuoni maarufu wa Makerere Ali Mazrui alikuwa na mtizamo tofauti.
Kwa maoni yake, chuo kikuu kilikuwa kinapoteza dira yake ya kukabiliana na changamoto za kijamii na kisiasa zinazoizunguka jamii, na kwamba chuo kilikuwa kinapoteza mwelekeo wa malengo yake makuu ya ubora.
Nae Walter Rodney kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam alikuwa akihimiza kuwepo kwa uhalisia wa chuo kutokana na mazingira yake.
Iwapo Mazrui alitilia shaka fikra ya Rodney ya umuhimu wa wasomi wa chuo kikuu, kuibuka kwa madikteta baada ya ukoloni umewafanya wasomi wasiwe na njia mbadala zaidi ya wao nao kuingia katika ulingo wa kisiasa.
Machafuko nchini Uganda kati ya miaka ya 70 na 80
Tamaduni za kisomi ambazo ziliibuka zilikabiliwa na changamoto.
Idi Amin Dada kuwatimua raia wenye asili ya Asia kulitoa idadi kubwa ya wasomi.
Wasomi wengi wa Makereere walikimbia na wengine kuuawa katika vurumai hiyo.
katika sherehe za miaka 100, Makerere inaikumbuka historia hii kwa kuandaa makongamano pamoja na mijadala ya wazi.
Frank Kalimuzo, mkuu wa Chuo cha Makerere alitoweka kipindi cha utawala wa Amin alikumbukwa kwa jengo la kitivo cha ualimu kupewa jina lake.
Wanafunzi wengi waliomaliza Makerere walijipata kama sehemu ya jeshi la ukombozi na baadae wakawa katikati kuijenga upya nchi yao.
Makerere ilikuwa mwathirika wa kwanza baada ya Benki ya dunia kubinafsisha elimu ya juu.
Makerere ilikuwa inachukua wanafunzi wengi kuliko uwezo wake wa kufundisha, na baadahi ya vitivo ambavyo vilikuwa havina wanafunzi viligeuka kutoa ushauri ili kupata fedha.
Mahmood Mamdani ameelezea hayo yote katika `Scholars in the Market Place.` Masoko nchini Uganda yana historia ya kuungua mara kwa mara.
Jengo ambalo ni alama ya kihistoria ya Makerere pia liliungua, na wakati kukiwa na sherehe za miaka 100, jengo hilo linajengwa upya.
Lakini Makerere imejifunza kwamba, ada pekee haitokshi kuendesha chuo, na hivyo, imetumia sherehe za maadhimisho ya miaka 100 kuongeza nguvu mfuko ujulikanao kama `Endowment Fund` ili kusaidia gharama za uendeshaji.
Hata hivyo, bado kuna wingu la usahaulifu.
Chuo kinaendelea kusahau mchango wake wa kupambana na ukoloni ambao kilichangia pakubwa.
Hata wakati ambapo Makerere imeadhimisha miaka 100 ya uwepo wake, imeendelea kusahau mchango sio tu wa wanawake waliopita Makerere ambao walidhulimiwa lakin hata wale ambao nyota zao ziling`aa.
Dk. Theresa Nanziri Bukenya, ambae alikuwa mtaalamu bingwa wa hesabu aliuawa kwa kupinga ukatili wa wanajeshi wa Amin, lakini habari yake haikuzungumzwa katika maadhimisho.
Mbali na wanawake kama vile Dk. Specioza Wandira Kazibwe ambae alipanda ngazi na kuwa makamu wa kwanza rais mwanamke barani Afrika.
Sasa hivi kuwepo kwa ushawishi wa jukwaa la kidigitali kama vile TRT AFRICA, matumaini yaliyopo ni kwamba wana Makerere bado wanaweza kuamka alfajiri na kutumia uwezo wao wa kubadilisha jamii.