Balozi Siwa amechukua nafasi ya Said Hussein Massoro ambaye, kabla ya kuteuliwa kuwa Balozi, alishikilia cheo hicho tangu Januari alipoandishwa cheo kutoka naibu mkurugenzi mkuu wa idara ya Usalama wa Taifa hadi mkurugenzi mkuu wa idara.
Mkurugenzi mkuu mpya wa TISS, Balozi Siwa, alikula kiapo kwenye Ikulu ya Dar Es Salaam chini uongozi wa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
Balozi mstaafu Siwa alihudumu kama mwenyekiti wa bodi ya wadhamini wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), wadhfa alioshikilia tangu uteuzi wake na marehemu Rais John Magufuli.
Mnamo mwaka wa 2014, Rais mstaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete alimteua balozi wa Tanzania nchini Rwanda hadi mwaka wa 2018.
Mkurugenzi mkuu huyo mpya amelihudumia Taifa la Tanzania tangu mwaka 1977 ambapo ameweza kushika wadhfa mbalimbali ikiwemo kwenye wizara ya mambo ya nje.
Kabla ya uteuzi wake kuongoza ubalozi wa Rwanda, Siwa alikuwa afisa wa mambo ya nje katika Ubalozi wa Tanzania, Abu Dhabi UAE, huku akitajwa kuhudumu katika balozi za Tanzania Urusi, na Berlin, Ujerumani.