Safari ya Yahaya Abdulai kutoka Ghana, nchini Uturuki ilianza alipojiunga na chuo kikuu cha Recep Tayyip Erdogan (RTEU), mjini Rize, baada ya kupata nafasi ya kusomea udaktari, 2018.
Abdulai, ambaye alijifunza Kituruki kupitia msaada wa RTEU na Muungano wa wanafunzi wa wa kimataifa, alishiriki katika maonyesho mbalimbali ili kujifunza kuhusu utamaduni wa eneo hilo huku naye akitambulisha utamaduni wake.
"Nimetoka Afrika, na nilijifunza utamaduni kama huu, ninacheza, na watu wanashangaa. Mimi pia ni mchezaji mzuri wa densi ya horon, bila shaka na wengi wao wanapenda." Abdulai alisema.
Mwanafunzi huyo, ambaye alizoea taifa la Uturuki, hakurejea nchini mwake hata wakati wa likizo, na hapo alianza kufanya kazi katika kituo cha utalii katika wilaya ya Çamlıhemşin, ili kukidhi mahitaji yake ya shule ndani ya wigo wa kazi iliyofanywa na idara ya Utamaduni na Utalii.
Aidha, baadaye Abdulai alijifunza densi ya horon ambayo ni sehemu muhimu zaidi ya utamaduni wa eneo hilo, na baadhi ya nyimbo za kitamaduni za atma katika eneo hilo.
“Mimi pia nilishangaa kwani kuna watu wanaandikia kutoka nje ya nchi na pia kila siku wafuasi wangu wanaongezeka. Nimekuwa nikifanya kazi hiyo kwa miaka 4, lakini video zimevutia sana.'' Alisema
Takriban mwaka mmoja uliopita, nyota ya Abdulai ilizidi kung'aa na hata kugeuka gwiji huku akiwafundisha watalii waliofika kwenye eneo hilo, densi ya horon. Alifanikiwa, na kuchukua jukumu hili kwa kutiwa moyo na mwendeshaji wa idara ya Utamaduni na Utalii eneo la Rize.
Kuanzia kipindi hicho, Abdulai, ambaye hucheza horon na kuimba nyimbo za kitamaduni za atma kwa watalii wanaotembelea mkoa huo, alianza kusambaza video zake kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii. Video za Abdulai, ambazo zimesifiwa sana, zimetazamwa zaidi ya milioni 1 kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii.
"Nilichapisha video kwenye ukurasa wangu mwenyewe na video ilitazamwa kwa mara milioni 1 ndani ya siku mbili. Nina furaha, ninajaribu kuweka utamaduni huu hai. Tunapenda utamaduni, tunajaribu kuudumisha kadri ya uwezo wetu." Abdulai alifafanua
Baadhi ya watalii wanaofika Rize, humtembelea Abdulai, ambaye wanamfahamu kupitia mitandao ya kijamii.
Yahaya Abdulai aliwaambia waandishi wa habari kwamba alitumia miezi ya kiangazi kufanya kazi huko Rize. Ameongeza kuwa amekuwa akifanya kazi katika hoteli moja na alijifunza kucheza horon na kuimba nyimbo za kitamaduni za atma kwa kutazama.
Yahaya sasa amekuwa mmoja wetu
Mhudumu wa hoteli mjini Rize, Uturuki, Hatice Kaptan alisema kuwa walikutana na Abdulai mwaka alipokuja Uturuki.
"Alianza kufanya kazi nasi na kujifunza utamaduni wetu haraka sana. Aliingia densi ya Horon kwanza kama mchezaji, lakini alianza kuwa stadi na kucheza kwa ubora zaidi.
Abdulai ni mtu anayeona haraka sana, anajifunza haraka sana.
"Pia alijifunza nyimbo zetu za kitamaduni za atma haraka sana. Nilipokuwa nikifanya kazi hapa, kulikuwa na kipindi chenye ongezeko la ushawishi wa mitandao ya kijamii. Katika msimu wa baridi, Abdulai alijulikana zaidi kwa kushiriki katika hafla mbalimbali. Kwa kweli amekuwa mwana wetu sasa."
Raia huyo wa Ghana amesema kuwa amekuwa akicheza na kuandaa video zake akishiriki densi ya horon kwa kutumia mitandao ya kijamii kwa kati ya miezi 5-6.