Maoni ya waafrika baada ya logo ya Twitter kutoka kwenye alama ya ndege na kupelekwa kwenye X

Maoni ya waafrika baada ya logo ya Twitter kutoka kwenye alama ya ndege na kupelekwa kwenye X

Je unafahamu ni jinsi gani watumiaji wa Twitter barani Afrika wamepokea muonekano mpya wa mtandao huo maarufu Duniani?
Mabadiliko ya nembo ambayo yalianza kutekelezwa Jumatatu ni sehemu ya mageuzi ya Twitter. Picha: Reuters

Na Charles Mgbolu

Mamilioni ya watumiaji wa Twitter ulimwenguni kote ambao wamependezwa na walipendezwa na nembo ya ndege ya bluu ya Twitter wanashangaa ikiwa ni kwanini Mmiliki wa sasa wa Twitter na Tajiri Elon Musk amefanya jambo lisilokuwa linategemewa.

Mabadiliko ya nembo ambayo yalianza kutekelezwa Jumatatu ni sehemu ya mageuzi ya Twitter.

Katika mfululizo wa tweets mwishoni mwa juma, Elon Musk alisema kuwa anapanga kubadilisha nembo ya Twitter kutoka kwa ndege maarufu hadi "X" kuashiria mabadiliko makubwa ya hivi karibuni tangu aliponunua jukwaa la mtandao wa kijamii kwa dola bilioni 44 mwaka jana.

‘’Natarajia kufanya kazi na timu zetu na kila mmoja wa washirika wetu kuleta mtandao wa X ulimwenguni,” Musk aliandika Jumapili kwenye ukurasa wake kwenye mtandao huo.

Mawazo tu ya mabadiliko hayo makubwa yalizua hisia kali kwenye mitandao ya kijamii, huku watumiaji wengi wakiona ni jambo la ajabu.

‘’Mmiliki wa Twitter Elon Musk ametangaza kuwa atabadilisha nembo ya ndege ya Twitter kuwa “X. Hata hivyo, Mask anajulikana na kufahamika kwa ucheshi wake,” aliandika mtumiaji wa Twitter anayeitwa Abduljelil Kawo kutoka Ethiopia.

Twitter 'haitotambulika'

Lakini hii haikuwa mzaha, na tangu tangazo hilo la kwanza kutoka kwa Musk, matukio ya ubadilishaji huo yamefanyika kwa haraka sana. Ndani ya chini ya masaa 24, Musk alilinganisha maneno yake na vitendo.

Afisa Mkuu Mtendaji wa Twitter Linda Yaccarino pia alitweet: ‘’Kwa miaka mingi, mashabiki na wakosoaji wamesukuma na kuhakikisha Twitter inakuwa na ndoto kubwa zaidi na kuvumbua haraka, na ili kutimiza Malengo yetu makuu tunaona kabisa X atafanya hivyo na huenda akafanya zaidi.''

Nembo mpya ya chapa ya Twitter ilionyeshwa moja kwa moja kwenye jukwaa siku ya Jumatatu, na kusababisha mamilioni ya mashabiki na watumiaji kushtuka kwani hawakuweza kuelewa ni kwa nini ndege maarufu wa bluu ameamua kuondolewa.

‘’Kwa nini?’’ aliuliza Nora Yeboah-Afari, mtumiaji wa Twitter kutoka Ghana. ‘’Ninaangalia nembo sasa, na sioni kwamba kama ipo sawa na haitoi, haijitangazi na hata haivutii kwani Inatoa muonekano tofauti sana, na inafanya Twitter kutotambulika,’’ aliiambia TRT Afrika.

‘’Kubadilisha nembo kutafanya nini? Je, hii itaathiri jina pia kwa sababu jina Tweets ni sawa na ndege? Ndiyo maana nembo hiyo ilikuwa ndege,’’ alisisitiza Mayowa Adegoke, Mbobezi wa mitandao ya kijamii kutoka Nigeria.

Zoezi la kawaida

Lakini mchambuzi wa kuhusu chapa na masoko Ade Adetunji anafikiri kwamba Elon Musk anaweza kuwa katika awamu za mwanzo za kucheza story za mpira mkubwa wa theluji ili kufanya na kuvutia zaidi watu huku akijiandaa na uuzaji wa hisa ili kubadilisha utajiri wa Twitter.

‘’Elon ni mtu ambaye anafanya mambo kwa kasi ya haraka sana, na kile ambacho ametoka tu kufanya kwa kubadilisha nembo ni kawaida na uchukuaji wa kampuni,’’ Adetunji anaiambia TRT Afrika.

‘’Ninaamini kutakuwa na mabadiliko zaidi yajayo, na nembo hii mpya inatarajiwa kuimarisha utambulisho mpya wa Twitter itakavyokuwa,’’ alisema.

Tangu Twitter imenunuliwa na Tesla na Afisa Mtendaji Mkuu wa SpaceX Elon Musk, programu imekuwa ikikabiliwa na dhoruba, huku kukiwa na kuachishwa kazi, mabadiliko ya sera, na mizozo ya kisheria ikisalia kuwa masuala yanayoendelea.

Changamoto kubwa zaidi, hata hivyo, imekuwa uzinduzi wa mtandao wa Threads kutoka kwa mpinzani wake Meta, ambayo ililazimisha Twitter kutishia hatua za kisheria juu ya kile ilichokiita programu ya "copycat", ikidai Meta ilitumia vibaya siri za biashara za Twitter na mali nyingine ya kiakili. Meta ilikanusha madai hayo.

Pia kuna shida za kifedha, Musk alitangaza mnamo Julai kwamba mapato ya kampuni yake yameshuka kwa takriban 50%, ikionyesha hitaji la dharura la kufikia mtiririko mzuri wa pesa.

Musk alinunua Twitter kwa milion 44 dola | Picha: AP

Bado kuna mashabiki wa kutupwa ambao hawako tayari kukubali mabadiliko haya.

‘’Twitter ndio nilikua nayo, na urekebishaji huu wa nembo, ingawa unakatisha tamaa, hauna nguvu ya kutosha kuniondoa kwenye programu,’’ anasema Nora.

‘’ Ilimradi tu ahifadhi msingi wa Twitter, ambao ni jukwaa la ujumbe ambalo hushiriki maandishi, picha, na video, hatapoteza masoko mengi,’’ Adetunji alisema.

‘’Ninaelewa hisia kali zilizoambatanishwa, lakini kwa vile mabadiliko huwa hayaepukiki, hatimaye watu watajifunza kuishi nayo,’’ alihitimisha Adetunji.

TRT Afrika