TikTok inatumiwa na maelfu ya Wasomali vijana. Picha Reuters

na

Charles Mgbolu

Watumiaji wengi wa TikTok wanaamini wanaishi katika ulimwengu wa uwezekano ambao wanapata mambo mengi nje ya maisha ya kawaida, ambapo wako huru kuwa chochote na kufanya kila kitu na kwa wakati wowote. Hiki ni kipengele cha kuvutia cha TikTok, mahali ambapo pamekuwa kimbilio kwa wengi, ulimwengu wa kidijitali wa rangi na jumbe mbalimbali za utani ambapo hakuna hofu, wasiwasi, changamoto, au maumivu ya moyo.

Kwa wengine, TikTok ni jukwaa la kuishi na kuonyesha umaridadi na maisha yao binafsi na vitu wanavyovimiliki mfano nyumba, gari na vyanzo tofauti vya mapato ambavyo kwa kawaida huwakoga watu.

Lakini TikTok inazidi kuchunguzwa, kiasi kwamba katika nchi zingine, ulimwengu huu mbadala wa Kidijitali umesimamishwa. Kusambaa kwa kupigwa marufuku Kwa watumiaji wa TikTok nchini Somalia, nchi ya hivi karibuni kupinga mtandao huo nchini humo kumeleta sintofahamu baada ya uamuzi huo kuja kwa mshangao miongoni mwa watu waishio Somalia.

TikTok imekua katika mapato ya utangazaji na idadi ya watumiaji. Picha AP

‘’Sasa mtandao huo hautatumika kwenye nyumba nyingi nchini humo kwa sababu ya marufuku ya TikTok,’’ anasema Abdullah Ali Mohammed mjini Mogadishu. ‘’Tunatoa wito kwa serikali kutopiga marufuku TikTok kwa sababu huko ndiko tunapata mkate wetu wa kila siku,’’ alisihi.

Kukua marufuku

Serikali ya Somalia ilikuwa "ikifanya kazi kulinda tabia ya kimaadili ya jamii ya Wasomali wakati wa kutumia zana za mawasiliano na mtandao," Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia wa Somalia Jama Hassan Khalif alisema.

''Jukwaa la kiteknolojia lilikuwa limeongeza kukuwa kwa tabia mbaya kinyume na maadili na mazoea mabaya,'' aliongeza.

Mahitaji ya biashara Muuzaji dhahabu wa Kisomali, Halimo Hassan, hata hivyo, anahoji kwamba kunapaswa kuwa na aina fulani ya kuzingatia kwa watu wanaopata riziki kwa kuuza bidhaa zao kwenye TikTok.

Mahitaji ya biashara

‘’ Marufuku ya TikTok itakuwa na athari kwa biashara yetu kwa sababu tunauza bidhaa zetu nyingi kupitia TikTok. Tunatangaza kwenye TikTok, na watu hutazama kutoka kote ulimwenguni. Watu kutoka nje ya nchi na wenyeji huja kwetu kupitia matangazo yetu ya TikTok. Na watu hutujia na picha tulizochapisha kwenye TikTok na kisha kununua kutoka kwetu,’’ anaeleza.

TikTok inakabiliwa na ushindani kutoka kwa wakubwa wengine wa mitandao ya kijamii. Picha AA

Kulingana na Benki ya Dunia, zaidi ya asilimia 20 ya watu wenye umri wa kufanya kazi nchini Somalia hawana kazi, huku mitandao ya kijamii ikiwa na ushawishi mkubwa na sehemu ambayo imebeba jukumu muhimu katika kusaidia kukomesha idadi hiyo.

Walakini, kuna baadhi ya Wasomali ambao wanabishana kuwa kupigwa marufuku kwa TikTok kutaleta sifa kubwa sana. ‘’Nimefurahishwa sana na kupigwa marufuku kwa TikTok, na ningependa kupigwa marufuku kwa mitandao mengine kama hiyo,’’ anasema Falis Ali, mkazi wa Mogadishu.

Kupigwa Marufuku kwa hivi majuzi kwa mtandao wa TikTok nchini Somalia kumezua tafrani, huku jukwaa la kamari la 1XBet likikabiliwa na Kesi na, likishutumiwa kwa kushusha maadili katika jamii.

TRT Afrika