Hijja ni nguzo ya tano katika dini ya Kiislamu, ibada ambayo inatakiwa kufanywa angalau mara moja katika maisha ya kila Muislamu/ Picha: AA

Baada ya msimu wa Hija wa mwaka 2023 uliofanikiwa, mamlaka za Saudi sasa zinajiandaa kwa msimu ujao wa Hija.

Tumeshuhudia maendeleo mengi mapya tangu janga la Uviko 19, na mwaka huu si tofauti, ikifanya urahisi wa kutembea na kuabudu, hali ambayo imewafanya baadhi ya watu kujiuliza ikiwa mambo ya kisasa na teknolojia vimewapokonya waumini ugumu wa kweli na uelewa wa hadithi nyuma ya Hajj.

Haya ndiyo mambo mapya katika Hajj ya mwaka huu nchini Saudi Arabia.

Saudi Arabia Yatangaza Nusuk Wallet kwa Mahujaji wa Umrah na Hija

Wizara ya Hija na Umra (MoHU) na Benki ya Kitaifa ya Saudi (SNB AlAhli) wamezindua Nusuk Wallet, mkoba wa kidijitali wa kwanza duniani kwa mahujaji wa Umrah na Hija, ukilenga kuboresha usimamizi wa kifedha kwa mamilioni ya mahujaji wakati wa kukaa kwao. Inawawezesha mahujaji kushughulikia fedha zao kwa urahisi wakati wa kukaa kwao ili kutekeleza ibada.

Nusuk Wallet

Nusuk Wallet inaruhusu usalama vya hali ya juu kama vile akili mnemba, uthibitishaji wa utambulisho kwa alama za kibayometriki, na usimbaji wa hali ya juu, ikiweka kiwango kipya katika uzoefu wa Hija na Umra.

Uzinduzi wake unalingana na maono mapana ya Saudi Arabia ya mabadiliko ya kidijitali, na kuahidi zana salama na rahisi ya usimamizi wa kifedha kwa mahujaji duniani kote.

Nembo mpya ya Mpango wa Njia ya Makkah

Mkurugenzi Mkuu wa hati za kusafiria ametambulisha chapa maalum inayoonyesha utambulisho wa kuona wa Mpango wa Njia ya Makkah.

Chapa hii, inayowekwa kwenye pasipoti, inatumika kama alama maalum kwa mahujaji wanaoshiriki katika mpango huo, ikirahisisha utambuzi wa haraka katika viwanja vya ndege mbalimbali. Inapatikana katika kumbi maalum katika viwanja vya ndege duniani, mahujaji wanaweza kufikia taratibu zilizorahisishwa kirahisi tu, kuboresha ufanisi wakati wa safari yao.

Chapa ya Makkah
TRT Afrika