Na
Charles Mgbolu
Tamasha la Kimataifa la Filamu la Marrakech nchini Morocco la mwaka 2023 limefika mwisho na kutangazwa kwa washindi wa tuzo zake mashuhuri katika hafla ya kufunga iliyopambwa na nyota mbalimbali mwishoni mwa wiki.
Tuzo ya kwanza, tuzo ya Etoile d'Or, ilitolewa kwa mtengenezaji filamu wa Morocco, Asmae El Moudir kwa kazi yake katika ‘’Mother of all lies."
Filamu hiyo ya kumbukumbu yani documentary inafuatilia hadithi ya mwanamke anayetafuta kwa udi na uvumba ukweli wa historia ya familia yake.
Ilionyeshwa kwa mara ya kwanza katika Tamasha la 76 la Filamu la Cannes, ambapo El Moudir alishinda Tuzo ya Filamu Bora ya Kumbukumbu akiwa pamoja na mtengenezaji filamu wa Tunisia, Kaouther Ben Hania.
Pia ilichaguliwa kama filamu ya Morocco inayowakilisha kipengele cha Filamu Bora ya Kimataifa katika Tuzo za 96 za Academy.
Tuzo ilitolewa kwa washindi wa nafasi ya pili na ya tatu, "Goodbye Tiberius" ya mwendeshaji wa Kipalestina Lina Soualem na "Wolf of the Wild" ya mwendeshaji wa Kimoroko Kamal Lazrak.
Mwendeshaji wa Kifaransa-Kisenegali Ramata-Toulaye Sy alishinda tuzo ya Mwendeshaji Bora, Director, kwa filamu yake Banel & Adama.
Asja Zara Lagumdzija alishinda Tuzo ya Mwigizaji Bora wa Kike kwa ajili ya drama ya Bosnia iitwayo Excursion, iliyoandikwa na kuongozwa na Una Gunjak, na Doga Karakas alishinda Tuzo ya Mwigizaji Bora wa Kiume kwa ajili ya filamu ya Kituruki iitwayo Dormitory iliyotengenezwa na Nehir Tuna.
Tamasha hilo lilionekana kama ishara ya ujasiri wakati Morocco inajaribu kushinda athari mbaya za tetemeko la ardhi lililopiga jamii za milimani zinazozunguka Marrakech mwezi Septemba.