Saa ya Dunia 2024: Taa zilizimika kwenye Mnara wa Eiffel huko Paris, Ufaransa saa 8"30 jioni kwa saa za ndani. / Picha: AA

Kama ishara ya kulinda mazingira ya sayari, baadhi ya majengo ya kihistoria duniani yalizima taa zisizo muhimu kwa saa moja kuitambua saa ya Dunia mnamo Machi 23.

Mnara mashuhuri wa Eiffel wa Ufaransa ulizima taa zake Jumamosi usiku (Machi 23) kutambua "Saa ya Dunia", ili kuangazia mabadiliko ya hali ya hewa.

"Zima taa, na uelekee ulimwengu wenye mustakabali mwema kwa wote," Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres alisema katika ujumbe wa tukio hilo.

Jengo la Empire huko New York, Marekani lilikuwa gizani wakati wa Saa ya Dunia ambayo pia inalenga kuongeza ufahamu wa dharura ya hali ya hewa na mabadiliko ya tabia nchi.

Saa ya Dunia 2024: Taa zilizimwa kwa dakika 60 katika jengo la Empire State huko New York, Marekani. / Picha: AA

Maeneo machache kutoka kwa jengo la Empire, taa pia zilizimwa kwenye jengo lenye ghorofa 40 kwenye Mto Mashariki kwa dakika 60.

"Hali ya hewa yetu inaharibika," Bw. Guterres alisema, na Saa ya Dunia "inaonyesha nguvu ambayo kila mmoja wetu anayo katika kupigania maisha yetu ya baadaye".

"Pamoja, tuzime taa na tuelekee kwenye ulimwengu wenye mustakabali mzuri kwetu sote," alisema.

Saa ya Dunia 2024: Giza la saa moja kwenye Hekalu la Parthenon huko Athene, Ugiriki kuashiria Saa ya Dunia. / Picha: AA

Huko Ugiriki, hekalu maarufu la Parthenon Temple pia liliingia gizani, likiongoza wito wa kimataifa wa kuzima taa saa 8.30 p.m. na kutumia dakika 60 kunufaisha sayari.

Mfuko wa Dunia Kwa ajili ya raslimali za asili (WWF), shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na uhifadhi, lilianza mpango wa kuzima taa huko Sydney, mwaka wa 2007.

Tukio hilo la kiishara la kuzima taa, limegeuka kuwa kichocheo kikuu cha kukuza harakati za ulinzi wa mazingira kwani ulimwengu sasa uko kwenye 'kikomo' cha misukosuko ya hali ya hewa na raslimali asili.

Saa ya Dunia 2024: Taa zinazimwa kwenye Mnara wa Galata huko Istanbul, Türkiye. /Picha: AA

Mnara wa Galata wa Uturuki ulioko Istanbul pia ulijiunga na kampeni hiyo ya kuzima taa katika zaidi ya nchi na wilaya 190 ulimwenguni.

Kulingana na WWF, zaidi ya 'saa 410,000 zilitolewa' kwa sayari mwaka jana na wafuasi katika zaidi ya nchi na maeneo 190.

Mwaka huu, waandaaji walinuia kufanya tukio la kila mwaka kuwa 'Saa Kubwa Zaidi kwa ajili ya Dunia' kwa kutumia dakika 60 kunufaisha sayari.

TRT Afrika