Malori 300 ya mchanga yalisafirishwa hadi kwenye kilele cha Erciyes kwa mashindano hayo. / Picha: AA

Kayseri, jimbo la kati la Anatolia la Uturuki, limekuwa mwenyeji wa mashindano ya kwanza ya mpira wa wavu ya ufukweni kwenye mlima, katika mita 2,200 kwenye Mlima Erciyes.

Mashindano hayo, yaliyoandaliwa kwa ushirikiano kati ya Manispaa ya mji wa Kayseri, Shirikisho la Mpira wa Wavu la Uturuki (TVF), na Kayseri Erciyes Inc yalishuhudia timu kumi na sita za wanaume na 13 za wanawake kutoka Uturuki, Ukraine, Iran, na Jamhuri ya Uturuki ya Cyprus Kaskazini zikichuana.

Kwa kawaida mchezo huo uliozoeleka kufanyika kwenye fuo za mchanga kando ya bahari, lakini wakati huu, mechi za voliboli ya ufuo, zilifanyika kwenye viwanja maalum vilivyotayarishwa kwenye Mlima Erciyes wa mita 2,200.

Hamdi Elcuman, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Erciyes Inc., alisema, "Kwa mara ya kwanza duniani, tunaandaa michuano ya mpira wa wavu ya milimani. Erciyes itaendelea kutoa huduma za utalii na michezo kwa jiji na eneo letu kwa muda wa miezi 12. ," alisema.

Mkurugenzi wa Mpira wa Wavu wa Ufukweni na Theluji wa TVF, Oguz Degirmenci, alidokeza kuwa tukio hili, linaloashiria historia ya mara ya kwanza kabisa mpira wa wavu wa ufukweni kuchezwa kwenye mlima, linatarajia matokeo ya kimataifa.

Washindi walitunukiwa zawadi za pesa taslimu, medali na vikombe

Katika kitengo cha wanaume, nafasi ya kwanza ilichukuliwa na Yusuf Ozdemir-Batuhan Kuru, akifuatiwa na Arash Vakili-Abdolhamed Mirzali katika nafasi ya pili, na Hasan Huseyin Mermer-Sefa Urlu katika nafasi ya tatu.

Katika kitengo cha wanawake, Bugra Eryıldız-Diana Lunina alipata nafasi ya kwanza katika kitengo cha wanawake, Merve Celebi-Esra Betul Cetin aliibuka wa pili, na Kseniia Mavzur-Anna Kolcenko aliibuka wa tatu.

TRT World