Mkutano ulipokamilika, adhana ilikaririwa ikiandamwa na tafsiri yake kwa Kiingereza. Picha AA

Meya Eric Adams ametangaza ya kwamba Jiji la New York litaruhusu adhana, mwito wa Kiislamu kwa sala, kutangazwa kwa nyakati zake zilizowekwa kila Ijumaa na wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

"Kwa muda mrefu sana, kumekuwa na mkanganyiko kuhusu jamii zipi haziruhusiwi kufanya wito wao kwa maombi," Adams alisema katika mkutano na wanahabari.

“Hii leo, tunakata kauli na kusema wazi kwamba misikiti na nyumba za ibada ziko huru kuongeza mwito wao wa kusali Ijumaa na wakati wa Ramadhani bila kibali muhimu,” alisema.

Katika kikao hicho na wanahabari uliohudhuriwa na wawakilishi kutoka makundi mbalimbali ya misikiti na taasisi za Kiislamu, Adams alisema: "Mko huru kutekeleza imani yenu katika jiji la New York kwa sababu, kwa mujibu wa sheria, sote tuna haki ya kutendewa sawa na utawala wetu unajivunia sana kufikia mafanikio haya."

Chini ya mwongozo mpya, msikiti wowote unaweza kutangaza adhana kila Ijumaa kati ya muda wa adhuhuri na vile vile kabla ya mlo wa kufungua saumu wa iftar kila jioni wakati wa mfungo wa mwezi wa Ramadhani.

Viongozi kutoka jamii ya Kiislamu walitoa shukrani kwa meya na maafisa wengine.

TRT Afrika na mashirika ya habari