Tuzo za mwaka huu zinadhaminiwa na kampuni ya simu ya Turkcell./Picha: AA

Maonesho ya maadhimisho ya miaka 10 ya Tuzo za Picha za Istanbul, zilizoandaliwa na Shirika la Anadolu, yataanza Istanbul Jumatatu.

Tukio hilo litahusisha picha bora zaidi nchini Uturuki.

Kwa kuongezea, kutakuwa na onesho kubwa linalohusisha picha bora zaidi kwa miaka 10.

Ikiwa imeandaliwa na maktaba ya Rami, onesho hilo litafanyika Juni 23, na kutoa fursa kwa wageni kufurahia taswira za matukio ya kidunia kwa mwaka uliopita.

Kuanzia kwa matukio ya mashambulizi ya Gaza hadi tetemeko kubwa la ardhi lililoikumba Uturuki mwaka jana, na matukio ya kihalifu ya nchini Mexico na janga la wakimbizi wa Afghanistan, picha hizo huonesha maisha halisi ya binadamu.

Sherehe ya ufunguzi wa maonesho hayo na uwasilishaji wa tuzo, chini ya ufadhili wa Mwenyekiti wa Anadolu na Mkurugenzi Mkuu Serdar Karagoz, itahudhuriwa na wanahabari kutoka kwa vyombo vya habari vya kimataifa.

Kwa mwaka huu, tukio hilo litadhaminiwa na kampuni ya simu ya Turkcell, huku kampuni ya Sony ikihusika na dhamini zawadi ya jumla.

Maelezo zaidi juu ya picha zilizoshinda tuzo hizo ziko kwente mtandao wa istanbulphotoawards.com.

TRT Afrika