Urejesho wa kumbukumbu ya muziki huo kwa njia ya kidigitali unadhihirisha weledi mkubwa wa sauti uliotumika kutunga nyimbo za kujenga taifa.
Ukitupia jicho taifa la Djibouti kwenye ramani ya dunia, ni taifa ambalo ni nadra sana kusemewa mengi zaidi ya eneo maalum la kimkakati, likiwa imeshikana na Ghuba ya Tadjoura, ndani ya Afrika ya Mashariki linaloonekana kuwa muhimu tu kwa ajili ya operesheni tofauti zikiwemo za kiusalama na kibiashara, kwa kuwa mkabala na bahari ya mediterranean na hivyo basi kuwa muhimu katika kuunganisha Afrika na Bara Asia.
Njia ya meli ya Bahari ya Shamu kwa miaka na mikaka imeifanya Djibouti kuwa sehemu muhimu ya ufanikishaji wa shughuli za kibiashara na eneo maalum la ubadilishanaji wa mila na desturi kutokana na mwingiliano wa watu kutoka jamii na matabaka tofauti; mwingiliano huu ukidhihirika zaidi kupitia Muziki.
Urithi huu wa utamaduni umekuwa moja kati ya siri kubwa zilizoweza kutunzwa mpaka 2019, wakati lebo ya Ostinato Records iliweka historia kwa kuwa chombo cha kwanza cha kigeni kupata fursa ya kuzuru hifadhi ya nyaraka za muziki wa Djibouti.
“Serikali ndiyo Lebo ya kurekodi,”alisema mwanzilishi wa Ostinato Vik Sohonie, akizungumza na TRT kutokea nyumbani kwake Bangkok.
“Muziki wa Djibouti ni wala ladha tamu. Hilo unagundua sio tu kwa aina ya muziki wanaozalisha lakini pia muziki walioshirikisha kutoka nje.”
Tangu mwaka wa 2016, Lebo hio ya Ostinato yenye makao makuu yake jijini New York imeachia albamu kutokea Haiti, Capeverde, Sudan na Somalia na ndipo Sohonie alipata fursa ya kupishana na muziki wa Djibouti akiwa kwenye harakati za kusaka haki za leseni za nyimbo mbili zenye asili yake Somalia. Nyimbo hizi ziliteuliwa kwenye Tuzo za Grammy 2017.
Shughuli za Sohonie zilimpelekea kuwasiliana na redio ya kitaifa nchini humo pamoja na televisheni ya Radiodiffusion-Television de Djibouti (RTD), na hapo baadae mamlaka husika zikamtambulisha kwa hifadhi ya nyaraka za muziki wanazopenda na kuenzi kama shirika.
Baada ya kuondoka kwake ikawa ni bayana kuwa Djibouti ni sehemu yenye utajiri mkubwa wa Sanaa na utamaduni na hivyo basi akaeleza washikadau wenzake juu ya hali halisi hio. Kufuatia majadiliano mapana ya miaka mitatu, lebo ya Ostinato ikapewa idhini na RTD kuchapisha kwenye majukwaa ya kidijitali zaidi ya kazi za muziki 5,000 zikiwemo kaseti.
Sehemu ya makubaliano baina ya Ostinato na shirika la RTD ilikuwa ni kurekodia shirika hilo kumbukumbu ya nyaraka, na ndani ya siku 3 studio ya kisasa ilikuwa tayari kwa ajili ya mchakato huo na kupekea kuzinduliwa kwa albamu ya kwanza ya kwanza ya kimataifa kutoka Djibouti kwa jina Dancing Devils of Djibouti.
Sohonie anaamini kuwa kazi hio inadhihirisha mbinu mpya ya kufahamu dunia miongoni mwa wasikilizaji.
“Kutokana na kile ambacho muziki huo unanieleza, basi watu wengi zaidi walitangamana katika sehemu hii ya dunia.”
“Kadri tunavyozidi kuifahamu Afrika Mashariki kwa kina, ndivyo tunavyong’amua zaidi kuwa muziki huu unapaswa kuwepo katika orodha za muziki na masafa ya redio kote ulimwenguni.”
Muziki kwa ajili ya kujenga taifa
“Machoni mwa wanahistoria wengi, Afrika baada ya kujinyakulia uhuru ni hadithi ya muziki. Baada ya ukatili wa ukoloni, mataifa ya Afrika yalikumbatia muziki kama mbinu moja ya mchakato wa kupigana kiroho na uchungu uliotokana na ukoloni.”
Wasanii hawakutumika tu na serikali kwa ajili ya propaganda, lakini kwa lengo la kukuza uzalendo na utangamano. Kikundi cha jazz cha Bembeya kutoka Guinea, Super Eagles ea Gambia na Orchestre Afrisa wa Congo ni baadhi tu ya mifano ya wasanii waliotekeleza jukumu hilo.
Vilevile, viongozi wa Djibouti waliamini kuwa muziki ni nguzo muhimu ya kuchochea utangamano na uzalendo wa taifa baada ya kujinyakua kutoka kwa minyororo ya Wafaransa mwaka 1977. Kadhalika jina 4 Mars – Quatre Mars kwa Kifaransa linatafsiriwa kama tarehe 4 Machi 1977, siku ambayo chama cha People’s Rally for Progress(RPP) kilianzishwa na baadae kuongoza serikali kama chama tawala tangu 1979..
Chama cha RPP kilianzisha bendi za muziki katika taasisi zote za umma kama njia moja ya kulileta taifa pamoja.
Kufuatia uchapishaji wa nyaraka za muziki wa Djiboutina lebo ya Ostinato katika majukwaa ya kidijitali, msururu wa muziki umefuata ikiwemo albamu tatu ambazo bado zinafanyiwa kazi na zitaonesha bendi tofauti kutoka Djibouti.
Kufuatia kuachiwa kwake rasmi Februari hii, Super Somali Sounds from the Gulf of Tadjoura ilizindua msururu wa kazi ya kikundi cha watu 40 kutoka ‘Somali supergroup 4 Mars’ waliorekodi nyimbo zilizowahi kutumbuizwa kwenye tamasha kati ya 1977 na 1994.
Sawia na Shirika la RTD, muziki wa 4 Mars’ vilevile unakumbatia muziki wa kisomali utokanao na mwingiliano mzuri wa tamaduni tofauti zilizotokea Djibouti zamani na kuongeza ladha ya sauti.
4 Mars inadhihirisha ladha ya muziki kutoka Sudan, Misri na Yemeni, mitindo ya kucheza ala za Uchina, Marekani, midundo ya Turkiye na Bollywood, reggae na Somali Dhaanto.
Sohonie anaamini utajiri huu wa muziki unawawezesha wasikilizaji kuelewa upya historia ya dunia. Swali ni Je, barabara zote zilielekea Roma ama zilielekea Ghuba ya Tadjoura?
Sohonie anadiriki kusema anauchukulia muziki kama chombo ya kuhadithia na kufunza historia mpya, kama nguzo ya maono na kazi yake ya muziki.
“Tukiamua kutumia muziki wa historia, tutabahatika sana kuleta pamoja matukio ya Afrika, Asia na Amerika ya Walatino, jambo ambalo litachochea fikra chanya miongoni mwa mataifa hayo kwa kuona muziki wao ukisherehekewa kwenye Jukwaa la Kimataifa.” Anasema Sohoine.
Na kwa hivyo basi kwa kuisikilizija historia ya Djibouti, Sohoine anatumai tutazingatia taifa hilo lenye mustakabali uliojaa matumaini.