Na Charles Mgbolu
Tamasha la Filamu la Tribeca limeweka wazi idadi ya filamu zitakazooneshwa kwenye tamasha hilo kwa mwaka huu.
Tamasha hilo huandaliwa kila mwaka na kampuni ya uzalishaji wa filamu ya Tribeca, likiangazia filamu, vipindi, mazungumzo, muziki, michezo, sanaa, na upangaji programu wa kina.
Kila mwaka, tamasha huandaa zaidi ya maonesho 600 na takriban watu 150,000 wanaohudhuria, na huwazawadia wasanii wa kujitegemea katika vipengele 23 vya ushindani.
Baadhi ya filamu za Kiafrika zimeingia kwenye safu hiyo ya kifahari inayotarajiwa kuanza Juni 5 hadi 16, 2024, huko mjini New York, nchini Marekani.
'Made in Ethiopia (Ethiopia)'
Ikiwa imetengenezwa nchini Ethiopia, filamu hii inasimulia hadithi ya mfanyabiashara aitwaye Motto, ambaye ana jukumu la kuzindua eneo la viwanda la China nchini Ethiopia. Filamu hiyo imeongozwa na Xinyan Yu na Max Duncan. Imetolewa na Tamara Dawit, Max Duncan, na Xinyan Yu.
Era Oculta – Hidden Era (Msumbiji)
Filamu hii imetengezwa katika jiji la Maputo, Msumbiji, ambapo msanii wa Rastafari Phambi anafanya kazi kusaidia elimu ya mtoto wake mchanga huku akipitia magumu ya kuishi maisha ya kisanii katika jiji lenye nguvu.
Imeongozwa na kutayarishwa na Carlos Vargas. Imeandikwa na Carlos Vargas na Franziska Ruess. Iliwashirikisha Paula Matlombe, Ednora Matlombe, Isac Tivane "Phambi," na Ixon Tivane.
Searching for Amani, (Kenya)
Kadiri ukame mbaya unavyoingia, ndio azma yake ya kumtafuta muuaji inabadilika huku uharibifu wa dhamana ya ulimwengu unaozidi kuwa wa joto unavyofunuliwa.
Searching for Amani imeongozwa na Nicole Gormley, Debra Aroko. Imetayarishwa na Peter Goetz, Mungai Kiroga, na Nicole Gormley.
The Weekend, (Nigeria)
Filamu ya kusisimua inamuangazia msichana yatima ambaye, huku akitamani familia, anatembelea familia ya mchumba wake inayoonekana kuwa na ustaarabu na kugundua siri yao mbaya.
Imeongozwa na Daniel Emeke Oriahi. Imeandikwa na Egbemawei Dimiyei Sammy, Vanessa Kanu, na Freddie O. Anyaegbunam Jr. na kutayarishwa na Uche Okocha.