Makthoum Abdalla, mmoja wa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Maarif, Sudan | Picha: Maarif

Na Nuri Aden

Katika mojawapo ya maamuzi ya kihistoria yaliyochukuliwa na Uturuki baada ya jaribio la mapinduzi lililofeli la kundi la kigaidi la FETO mnamo Julai 15, 2016, ilikuwa ni ndoto za mamilioni ya watoto barani Afrika ziliozokuwa zikisubiri kunusuriwa kutoka kwa itikadi potofu inayoenezwa na FETO.

Mtandao wa FETO, zikiwemo shule zilizoendeshwa na kundi hilo kama sehemu ya mbinu zake za kigaidi, umekuwa ukisambaratika katika misingi ya elimu barani Afrika tangu miaka ya 1990, kabla ya usiku wa giza kabisa katika historia ya kisiasa za Uturuki hivi karibuni, kusababisha hatua ya mageuzi ya kunusuru mustakabali wa vizazi katika bara zima.

Ikiitikia wito wa Rais Recep Tayyip Erdogan, pamoja na makubaliano ya pande zote kati yake na nchi za Kiafrika, mnamo mwaka wa 2016, Taasisi isiyo ya faida ya Maarif inayomilikiwa na Uturuki, ilichukua jumla ya shule 126 katika nchi 16 za Afrika ambazo zilikuwa zikiendeshwa na kundi la kigaidi la FETO.

Rais wa Taasisi ya Elimu ya Maarif, Prof. Birol Akgun. Picha: Taasisi ya Maarif

Watoto waliohitaji kuokolewa kutoka kwa mafundisho ya kigaidi ya FETO walianzia kiwango cha chekechea hadi sekondari. Mabadiliko hayo yaliwezekana kupitia historia ya ushirikiano kati ya Uturuki na mataifa rafiki ya Kiafrika.

Imepita miaka saba tangu serikali ya Uturuki ilipoanzisha hatua hii, na kuwawezesha mamilioni ya watoto barani Afrika kuendelea na masomo yao bila mawazo ya kisiasa ya FETO na kugeuza Wakfu wa Maarif kuwa kichocheo cha kusaidia uhusiano thabiti kati ya Uturuki na mataifa ya Afrika.

Wanafunzi wa Maarif nchini Somalia. | Picha: Taasisi ya Maarif

Taasisi ya Maarif—ambayo jina lake linatokana na neno la Ottoman-Kituruki la elimu au neno la Kiarabu la maarifa au hekima—ilianzishwa kama msingi wa elimu usio wa faida mnamo Juni 17, 2016 kupitia sheria maalum iliyopitishwa na Bunge la Kitaifa la Uturuki.

Kwa miaka mingi, Maarif imekuwa nguzo muhimu ya maendeleo ya Afrika kupitia elimu, kwa kutumia utaalamu wake wa kubuni mtaala bora na kutoa mafunzo yanayoendana na mahitaji mahususi ya kila nchi inakofanyia kazi.

Maarif huwapa wanafunzi elimu katika masomo ya msingi kama vile sayansi, hisabati, na sayansi ya kijamii, kuwapa ujuzi wanazohitaji ili kukabiliana na changamoto za siku zijazo, bila kuwafundisha vijana kiitikadi kwa ajenda zao za kisiasa, hii ikiwa tofauti kubwa kinyume na mbinu na itikadi potovu za shirika la kigaidi la FETO.

Rais wa Uturuki Erdogan akiwa na Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AU), Moussa Faki Mahamat

Somalia ilikuwa nchi ya kwanza kuikabidhi Maarif zaidi ya shule saba zilizokuwa zikimilikiwa na kundi la FETO, ikionyesha imani ya serikali katika taasisi hiyo ya Maarif.

Maarif imejizolea umaarufu nchini Tanzania kutokana na mchango wake katika sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na kusimamia zaidi ya shule 10 zenye zaidi ya wanafunzi 2,000.

Shule za Maarif pia zimekuwa zikiongoza kwa mtaala wao wa kipekee wa kujenga utambulisho unaozingatia tamaduni za Kiafrika, zikiwemo lugha mbalimbali za Kiafrika pamoja na Kituruki.

Taasisi ya Maarif inayoongozwa na serikali imepata umaarufu kutokana na uwezo wake wa kuwahami wanafunzi ipasavyo na zana za kina za kujikinga vilivyo dhidi ya itikadi mbovu za kisasa zilizoenea ulimwenguni wa leo.

Taasisi ya Maarif imesifika kwa kuwakinga watoto dhidi ya itikadi mbovu za kisasa zilizoenea ulimwenguni wa leo. PIcha: Taasisi ya Maarif

Ikiongozwa na lengo la kulea wanafunzi wema, Taasisi ya Maarif imeendeleza juhudi zake za elimu katika vituo 447 vya elimu katika nchi 51, ikiwa pamoja na kuendesha shule za mafunzo stadi ya ufundi. Zaidi ya wanafunzi 50,000 ndani mataifa hayo, wanapokea elimu rasmi na mafunzo katika nyanja mbalimbali, pamoja na mafunzo ya ufundi stadi, kutoka taasisi ya Maarif.

Maelfu ya walimu na wafanyakazi wengine pia ni sehemu ya maafisa wa kutoa mafunzo. Shule za Maarif zinazidi kuvutia kote barani Afrika. Mahitaji kwa Shule za Maarif miongoni mwa taasisi nyingine za Uturuki huongezeka kila mwaka.

Taasisi ya Maarif imesifika kwa kuchangia kwa kiasi kikubwa kukuza vipaji vya watoto. Kupitia ushirikiano wa karibu, hasa na wizara za elimu katika nchi ambako inapatikana, Maarif inasaidia kwa kutoa ufadhili wa masomo ya bure kwa watoto wenye vipaji. Hatua hii hutumika kama aina ya uwajibikaji wa umma kupitia utoaji fursa kwa watoto wenye talanta teule kutoka Afrika.

Mama wa taifa wa Uturuki Emine Erdogan akiwa na wanafunzi wa mojawapo ya Shule za Maarif nchini Mauritania

Serikali ya Uturuki inazidi kutetea ulimwengu wenye usawa zaidi na wenye usalama kutoka mtazamo finyu kwa ujumla wa Afrika kama bara lililo tofauti na wenzake.

Taasisi ya Maarif inalenga kupanua upatikanaji wa viwango vya elimu ya kisasa kwa ulimwengu mzima. Hii inaiweka Maarif katika mstari wa mbele, na mchango wake isiyo kwa faida na ajenda wazi tofauti na shule za FETO ambazo zinaendesha biashara ghushi kote ulimwenguni.

"Kwa hakika, mafanikio ya ushirikiano wa kielimu ya Afrika na Uturuki kupitia Taasi ya Maarif chini ya Shule zake, ni jambo la kujivunia na kuendeleza ushirikiano bora na mustakabali bora kati ya Afrika na Uturuki." Anasema Profosea Dkt. Birol Akgun.

Kupitia mpango wa ufadhili wa serikali ya Uturuki katika elimu , zaidi ya wanafunzi 1,000 wa kiafrika huwasili Uturuki kila mwaka ili kujiandikisha katika vyuo vikuu vya Uturuki na kuendeleza masomo yao.

Kulingana na Prof. Birol Akgun, rais wa Taasisi ya Elimu ya Maarif nchini Uturuki, Maarif imechangia uhusiano wa kitamaduni kati ya Uturuki na Afrika. Ili kutimiza matakwa ya jumuiya ya Kiafrika na kuunga mkono muingiliano wa kiuchumi, kijeshi na kisiasa na Uturuki, alisisitiza kwamba msingi huo unalenga kutekeleza matakwa ya watu wa bara hilo.

Somalia ilikuwa nchi ya kwanza kukabidhi kwa Maarif zaidi ya shule saba zilizokuwa zikimilikiwa na FETO. Picha: Maarif Foundation

"Tunafanya bidii sana kujenga uhusiano. Kiwango cha ukuaji wa viwanda na kufaulu kwa elimu nchini Uturuki, ni mojawapo ya mfano wa kuigwa kwa mataifa mengine ya Afrika.

Huko Togo, taasisi ya Maarif pia imeanzisha uwanja wa michezo wa kisasa wa Maarif kwa lengo la kuanzisha itifaki kuhusu ushirikiano na vilabu vya michezo kutoka Ligi kuu ya Soka ya Uturuki, vyuo vya michezo na vyuo vikuu vyenye kitivo cha sayansi ya michezo, kubadilishana uzoefu, msaada wa kiufundi, kuandaa michezo tofauti pamoja na shughuli za kuimarisha ushirikiano.

"Tunafanya juhudi kubwa kuwa sehemu ya mahusiano. Miundombinu ya Uturuki ni mfano wa kuigwa kwa nchi za Afrika kwa kiwango kilichofikia katika nyanja ya maendeleo ya viwanda na elimu." Profesa Birol Akgun alisema.

Tuzo za Maarif

Taasisi ya Maarif ilipokea tuzo kuu kutoka kwa Wizara ya Elimu ya Djibouti katika mwaka wa kalenda ya elimu ya 2018-19.

Aidha, wanafunzi wa Tunisia kutoka Shule ya Maarif, walitwaa tuzo maalum kutoka kwa majaji, Katika mashindano ya timu 73 ya roboti ya kwanza ya ligi ya Lego Arabia ya 2019, iliyoandaliwa nchini Jordan na Kituo cha Ubora katika Elimu na Jumuiya ya AI ya Roboti za Kiarabu.

Mwezi Disemba mwaka jana, zawadi ya programu bora ya baiolojia na mradi wa "Comparison of Hydroponic and Soil Plant Growth" ilikwenda kwa Shule ya Uturuki ya Maarif ya Zanzibar.

Maheen Masoud, mwanafunzi wa shule ya sekondari katika Shule ya Pak-Turk Maarif katika wilaya ya Lahore ya Pakistani, alishinda shindano la Hisabati la "O-Level Board" mnamo Juni 2021.

Mbali na hayo, Shule za Maarif nchini Niger pia zilijinyakulia Tuzo ya Afya, Usafi na Elimu Bora, na kuzishinda taasisi zingine kadhaa.

Pia, Maarif hushirikiana na vyuo vikuu vya Uturuki kuwapa wanafunzi elimu ya juu.

Hadi leo, takribani wanafunzi elfu kumi wa kiafrika wamehitimu masomo ya juu kutoka taasisi za kielimu za Uturuki. Mpango wa fursa ya udhamini wa kielimu umesaidia karibu wanafunzi 15,000. Takwimu hizi zinaonyesha kuongezeka kwa ukaribu na urafiki kati ya Uturuki na Afrika kila siku.

"Tutazidi kuimarisha undugu wetu na mataifa ya Afrika kwa uaminifu." Rais Erdogan amesema katika mkutano wa ushirikiano kati ya Uturuki na Afrika ulioandaliwa Istanbul mwishoni mwa mwaka 2021.

"Ni kweli kwamba mafanikio ya Elimu ya Uturuki kupitia Shule za Maarif na ushirikiano wa tasnia ya elimu ya Uturuki inatupa sababu za kujivunia na kusaidia kuboresha uhusiano na mustakabali bora kati ya Afrika na Uturuki." Prof. Birol Akgun alisema.

TRT Afrika