Staa wa bongo fleva Ali Kiba. Picha: Simba SC Tanzania

Wimbo mpya wa msanii wa muziki Afrika Ali Kiba alioutunga kwa ajili ya klabu ya ligi kuu ya Tanzania Simba, maarufu 'mnyama', umevuma kwa kasi na kutazamwa takriban mara nusu milioni ndani ya saa 24 kwenye ukurasa wa YouTube.

Kibao hicho kimefuta rekodi wa wimbo uliotungwa na Diamond Platnumz kwa ajili ya Simba maarufu 'Simba'.

Wimbo huo, 'mnyama', umevuma kwa kasi na kutazamwa takriban mara nusu milioni ndani ya saa 24 pekee kwenye ukurasa wa YouTube ikilinganishwa na wimbo uliotungwa na Diamond Platnumz kwa ajili ya Simba mwezi Agosti 2020 na kutazamwa zaidi ya mara milioni mbili ndani ya muda wa miaka miwili.

Kwenye Ukurasa wa Diamond, wimbo huo ulivutia 4,186 Comments, huku kibao cha Kiba cha Mnyama kikipokea maoni 4,712 ndani ya siku moja tangu kuachiliwa kwake, kufikia mwisho wa uandishi wa habari hii.

Nimepata mapokezi makubwa Simba, moyo unapenda unapo thaminika. Kiukweli nilikuwa nawaonea wivu sana Wanasimba. Asanteni kwa kunikaribisha

Ali Kiba

Alikiba alitangaza rasmi kuhamia wekundu wa msimbazi huku akielezea furaha yake ya kujiunga na klabu hiyo maarufu, sio tu Tanzania bali Afrika nzima. Ujio wa 'King Kiba' umechangamsha maandalizi ya siku ya Simba day huku rangi nyekundu ikitamba kwa ajili ya sherehe hizo.

Klabu ya Simba FC imemtangaza Ali Kiba kuwa mtumbuizaji mkuu kwenye hafla ya Simba day iliyoratibiwa kufanyika jumapili hii latika uwanja wa kihistoria wa Benjamin Mkapa.

Msanii huyo Ali kiba hakuchelea kuimiminia klabu ya Simba kwenye wimbo wake huku akiimba;

we unamjua Simba mnyama, Kwa vikombe vingi mnyama, Anaupiga mwingi mnyama mnyama, Sio leo toka zamani, Mnyama hana mpinzani.

Ai Kiba

Haya yanajiri siku chache tu baada ya wachezaji wa klabu ya Simba kurejea Tanzania kufikia tamati ya kambi yao ya maandalizi kwa minajili ya msimu ujao, jijini Ankara, nchini Uturuki.

TRT Afrika