Na Sylvia Chebet
Takwimu zilizokusanywa na Shirika la Afya Duniani zinaonyesha kuwa janga la Upweke linaharibu dunia, kwa kasi na bila ubaguzi. Upweke na kutengwa kwa jamii sasa ndio sababu ya vifo vingi duniani.
"Upweke unaathiri pakubwa afya na ustawi," Alana Afisa, mkuu wa kitengo cha mabadiliko ya idadi ya watu na afya ya uzee wa Shirika La Afya Duniani anaiambia TRT Afrika.
"Ushahidi uliopo unaonyesha kuwa ukosefu wa ukaribu na kijamii kwa kweli unabeba hatari kubwa ya kifo cha mapema kuliko sababu zingine za hatari zinazojulikana kama vile kuvuta sigara, unywaji pombe kupita kiasi, kutofanya mazoezi ya mwili, kunenepa kupita kiasi, na uchafuzi wa hewa."
Wataalamu wanasema upweke, halisi au unaodhaniwa, huongeza hatari ya mtu kujiua, kiharusi, wasiwasi, shida ya akili hususani afya ya akili na magonjwa mengine. Shirika la Afya Duniani linasema Upweke unaongeza hatari ya ugonjwa wa moyo na mishipa kwa 30%.
Shirika la Afya Iinafafanua kutengwa kwa jamii kama kuwa na idadi isiyotosha ya mtaji wa watu au jamii.
Kinyume na dhana kwamba wazee katika mataifa ya Magharibi wanateseka zaidi na kutengwa na jamii na upweke, hali hiyo huathiri watu wa rika zote duniani kote.
"Takriban 25% ya wazee duniani kote wanapata kutengwa na jamii na upweke, wakati 5-15% ya vijana wametengwa na jamii," anasema Alana, akinukuu matokeo ya utafiti wa Shirika la Afya Duniani.
Ingawa inaweza kuwa ya kushangaza, kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa, takwimu hizi zinaweza kuwa za chini. Bado, wanaangazia Upweke na athari zake ambao ukikosa uangalizi husababisha madhara makubwa kama kutakosekana uangalizi wa haraka.
"Watu wengi hupatwa na upweke, jambo ambalo linaweza kudhuru sana," Alana anaonya.
Shirika la Afya Duniani limeunda tume mpya ya uhusiano wa kijamii kushughulikia upweke kama tishio kubwa la kiafya, kukuza uhusiano wa kijamii kama kipaumbele.
Tume ina mamlaka ya miaka mitatu, ambapo itaangazia jinsi uhusiano wa kijamii unavyoboresha ustawi wa jamii na jamii na kusaidia kukuza maendeleo ya kiuchumi, maendeleo ya kijamii na uvumbuzi.
"Ninatumai kwamba kupitia kazi ya tume, watu wanaweza kutambua vyema zaidi wanapopitia upweke na kutengwa na jamii na kutambua kwamba kuna kitu ambacho tunaweza kufanya kuhusu hilo," Alana anaiambia TRT Afrika.
Wataalamu wamebainisha kuwa mtu anaweza kuwa na mtaji wa kijamii , kuolewa au kuishi katika familia yenye vizazi vingi, lakini bado akajihisi mpweke.
"Wazo hili la kuwa na mtaji wa watu au mtaji wa jamii inayokuzunguka unatokana na jinsi unavyohisi kuwa karibu na kuunganishwa na wengine, iwe katika eneo lako la kazi, ujirani, au jamii," Alana anaelezea.
Wakati watu hawapati usaidizi inapohitajika zaidi, kuna uwezekano wa kutengwa na jamii.
Alana anasema hii hutokea wakati msaada wa kihisia au kimwili, au hata mahusiano ambayo mtu anayo yatakuwa yamepungua au kuzorota
Kwenye sehemu yoyote hali inayokosesha furaha ya watu inaweza kusababisha matokeo duni ya kiuchumi. Kuhisi kutengwa na kutotegemezwa katika kazi kunaweza kusababisha kutosheka na utendaji duni wa kazi. Kuacha au kufukuzwa kazi kunaweza kufuata.
"Unapotambua kwamba huna furaha, kwamba haufurahii kiwango au ubora wa mahusiano yako, ni muhimu kufanya kitu kuhusu hilo," Alana anashauri, akikubali kwamba wakati mwingine inaweza kuwa vigumu zaidi kuliko inavyofikiriwa.
Chapisho la mkuu wa Shirika la Afya Duniani Dr Tedros Adhanom kwenye mtandao wa X linakubali uzito na ukubwa wa changamoto ya upweke. "Tunahitaji kulizungumzia kwa uwazi zaidi kuhusu jambo hili anaandika.
Miongoni mwa vijana, kutengwa kwa jamii kunaweza kusababisha matokeo duni ya elimu. Kulingana na Shirika La Afya Duniani ushahidi unaonyesha kwamba vijana wanaokabiliwa na upweke katika shule wana uwezekano mkubwa wa kuacha chuo kikuu.
Mjumbe wa vijana wa Umoja wa Afrika, Chido Mpemba, mwenyekiti mwenza wa tume hiyo anabainisha kuwa "barani Afrika na kwingineko, ni lazima tufafanue upya simulizi kuhusu upweke. Uwekezaji katika uhusiano wa kijamii ni muhimu katika kujenga uchumi wenye tija, uthabiti na dhabiti ambao unakuza ustawi wa watu. kizazi cha sasa na kijacho".
Alana anasema inaweza kusaidia kupata usaidizi kutoka kwa mtu mwingine au kuchukua hatua ndogo kama vile kubadilisha muda kwenye mambo mbalimbali ufanyayo "Badala ya kutuma ujumbe mfupi kwa mtu, piga simu hiyo," anahimiza.
Suluhu zingine za vitendo ni pamoja na kutumia wakati mzuri zaidi na familia na marafiki. Alana pia huwahimiza watu binafsi kushiriki katika shughuli zinazowezesha kukutana na kijamii zaidi au bora zaidi.
"Unaweza kujiunga na kikundi, klabu, kitu ambacho unavutiwa nacho, tafuta kitu kipya cha kufanya," anashauri, akiongeza kuwa "kusalimia majirani au kushirikiana na muuza duka wa eneo lako" kunajumuisha ishara za kusaidia.
Kujitolea, pia, kunasaidia kupunguza kutengwa kwa jamii. Wazo la kuunga mkono jirani au mtu mwingine "huelekea kukupa hisia ya kujisikia kushikamana vizuri", anasema Alana.
Wakati ulimwengu unasubiri mapendekezo ya Tume ya Upweke, kuna haja ya kukumbatia hatua ambazo tayari zimethibitishwa kusaidia. Uingiliaji kati wa kisaikolojia kama vile tiba na ushauri ni mzuri, na watu hawapaswi kusita kutafuta usaidizi kama huo.
Mbinu za kusaidia watu wanaopitia upweke na kutengwa na jamii zinahitaji kufikiwa zaidi.
"Kwa kuzingatia madhara makubwa ya kiafya na kijamii ya upweke na kutengwa, tuna wajibu wa kufanya uwekezaji sawa katika kujenga upya muundo wa kijamii wa jamii ambao tumefanya katika kushughulikia masuala mengine ya afya ya kimataifa, kama vile matumizi ya tumbaku, unene na uraibu," Daktari mkuu wa upasuaji wa Marekani, Dk Vivek Murthy, mwenyekiti mwenza wa tume hiyo anasema.
"Pamoja, tunaweza kujenga ulimwengu usio na upweke, afya na ustahimilivu zaidi."