Uchunguzi unaonyesha kuwa 48% ya watu barani Afrika wangekabiliwa na janga la kifedha ikiwa wangehitaji upasuaji. Picha: Nyingine

Na Sylvia Chebet

Bili moja tu ya hospitali baada ya matibabu inatosha kumuingiza mtu ndani ya shimo ya umasikini na madeni — msemo huu wa kutisha ni kweli kwa watu wengi katika nchi zenye kipato cha chini na kuliko mtu anavyoweza kufikiria.

Idiba Loudy Diane, mzawa wa Gabon, anajua maana ya kukabiliana na pigo ya aina mbili la ukosefu wa ajira na ugonjwa unaolemaza ambao ulimaliza akiba yake kwa haraka.

Matatizo yake yalizidi kuwa mabaya mnamo 2021 wakati hoteli aliyofanyia kazi huko Libreville ilipofungwa. Ifikapo mwaka 2023, alikuwa akielea kwenye kingo za umaskini bila kipato na mzigo wa gharama kubwa ya matibabu kwa ugonjwa wa figo toka utotoni.

"Kila kitu kilikuwa kigumu. Nilikuwa napata homa ya mara kwa mara, kutapika na uchovu," anasimulia kwa TRT Afrika. "Nililazwa hospitalini kwa mwezi mmoja. Figo zangu zilikuwa zimeacha kufanya kazi, na nilipata magonjwa mengine ya mapafu. Pia nilikuwa kwenye matibabu ya figo (dialysis)."

Huko Gabon, ziara moja ya matibabu ya dialysis hugharimu franc 200,000, sawa na dola za Marekani 325. Kwa Diane, gharama za matibabu zilizidi kuongezeka zikawa haziwezi kudumishwa.

Zaidi ya bili za hospitali, gharama za usafiri kwenda na kutoka kwa vituo vya huduma ya afya, wagonjwa wengine pia hupoteza mapato. Picha: Reuters

"Sehemu ngumu zaidi ilikuwa kwenda kwenye matibabu ya mara kwa mara. Nauli ya teksi ni ghali, na nilikuwa napata dialysis mara tatu kwa wiki," anasema Diane.

Familia yake ilijitokeza kuhakikisha matibabu yake yanaendelea, lakini si wote wana bahati ya kuwa na mtu wa kurejelea baada ya kuvunja benki katika dharura ya kimatibabu.

Maradhi Yaliyosambaa

Tafiti nyingi za Shirika la Afya Duniani (WHO) na Benki ya Dunia zinatambua jinsi "gharama za afya zilizo kubwa mno" zinavyolemea idadi ya watu katika nchi zinazoendelea.

Barani Afrika, wataalamu wa afya wana wasiwasi kwamba idadi kubwa ya watu inaweza sababisha wapoteze kila kitu baada ya maradhi makubwa yanayohitaji mtu kulazwa hospitalini kwa muda mrefu na ufuatiliaji wa hali ya juu.

Ifikapo mwaka 2020, ilikadiriwa kuwa asilimia 48 ya watu barani wanaweza kukumbwa na janga la kifedha ikiwa wanahitaji upasuaji.

Hata wakati wa kukabiliana na magonjwa ambayo hayahitaji upasuaji, wagonjwa wengi wamelazimika kuuza mashamba au mali zao kulipia huduma matibabu.

Utafiti uliofadhiliwa na WHO hivi karibuni ulifichua kuwa asilimia 55 ya wagonjwa wa kifua kikuu na kaya zao katika nchi 135 zenye kipato cha chini na cha kati walilazimika kutumia takribani asilimia 20 ya matumizi ya kila mwaka ya kaya kwa matibabu ya mwanafamilia mmoja.

Matatizo yake yalizidi kuwa mabaya mnamo 2021 wakati hoteli aliyofanyia kazi huko Libreville ilipofungwa. Ifikapo mwaka 2023, alikuwa akielea kwenye kingo za umaskini bila kipato na mzigo wa gharama kubwa ya matibabu kwa ugonjwa wa figo toka utotoni. 

Kulingana na wataalamu, pale ambapo gharama ya kaya moja kwenye masuala ya afya yanazidi asilimia fulani ya uwezo wake wa kulipa, na kupunguza matumizi ya mahitaji mengine ya msingi, hio inajulikana kama gharama kubwa.

Mbali na gharama za moja kwa moja za kimatibabu, mzigo unajumuisha kupoteza ajira, gharama za usafiri wa kwenda na kurudi katika vituo vya afya, na bei ya chakula.

TB Alliance, shirika lisilo la faida linalojitolea kugundua, kuendeleza na kutoa dawa za kifua kikuu kwa wanaohitaji, linasema wagonjwa wanaokataa dawa na familia zao wanapata wakati mgumu zaidi kukabiliana na ugonjwa huo.

Afrika Kusini, wagonjwa wengi wanaopambana na kifua kikuu, hasa katika kaya zenye kipato cha chini, wanakabiliwa na changamoto ya kupata si tu chakula chochote bali mlo sahihi na wenye lishe kuimarisha kinga yao.

"Wagonjwa walio chini ya dawa za kifua kikuu wanapata maumivu ya njaa pamoja na maumivu ya tumbo," Zani De Wit, afisa wa uhusiano wa jamii katika Taasisi ya Mapafu ya Chuo Kikuu cha Cape Town anaiambia TRT Afrika.

"Pamoja na viwango vya juu vya ukosefu wa ajira vinavyoongezeka, hali za kuishi zilizojaa watu, uhalifu na vurugu, Afrika Kusini pia inakabiliwa na mgogoro wa matumizi ya dawa za kulevya. Wagonjwa wanatumia dawa kama njia ya kutoroka changamoto za maisha ya kila siku."

Kwa sasa, programu nyingi za TB barani zinaungwa mkono na serikali na wafadhili kupunguza mzigo kwa wagonjwa.

Lakini kama anavyobainisha Zani, hali ya kifedha ya familia inaweza kuwa chini ya shinikizo kiasi kwamba "wagonjwa wataacha matibabu yao ya TB makuudi ili kuhakikisha wanapata ruzuku kwa ajili ya maisha yao".

Mbali na changamoto za kifedha, wagonjwa wa TB wanapata shida ya kupambana kihisia na kisaikolojia kukubaliana na ugonjwa wao mpya.

Wagonjwa wanaopambana na magonjwa mbalimbali wanaelewa pambano hili, hata serikali zikiendelea kufanya mipango ya kujenga kinga kwao kupitia bima ya afya kwa wote.

TRT Afrika