Viazi vitamu/ Photo: Getty Images

Na

Firmain Eric Mbadinga

Chakula chenye asili ya mizizi kimekuwa sehemu muhimu ya lishe tangu zama za wawindaji-wakusanyaji, huku kukiwa na juhudi ya kutafuta wa aina ya mbegu mpya na bora.

Nchini Burkina Faso, watafiti wamefanikiwa, baada ya utafiti wa kimaaabara maabara kukuza aina mpya ya mbatata tamu ambayo ina manufaa mengi zaidi ya ladha ya mdomoni.

Watafiti hao wanasema kuwa aina hiyo ya viazi vyenye utamu kama machungwa huleta virutubisho zaidi kuliko aina ya kawaida, inahitaji miezi mitatu tu kukomaa, na haina madhara yoyote ya kiafya.

Aina hio ya mbatata imegunduliwa na taasisi ya Institut de Recherche en Sciences de la Santé huko Bobo-Dioulasso mwezi Novemba mwaka huu kama mojawapo ya suluhisho la kuwaondolea wananchi hofu ya tatizo chakula.

"Ingawa kiasi cha uvunaji kwa hekta bado hakijapimwa, zao hilo linawakilisha mbadala wa ukosefu wa ngano katika soko la kutokana na mizozo ya kimataifa inayoendelea," Dk. Koussao Somé, kiongozi wa timu ya utafiti, aliwaambia maafisa kutoka wizara ya elimu ya juu, utafiti, na ubunifu katika hafla ya ufunguzi.

Changamoto ya kujitosheleza

Mamlaka zinafanya kazi ili kudumisha usalama wa chakula katika kanda. Picha: TRT Afrika

Mwaka 2024, suala la kujitosheleza kwa chakula litabaki kuwa changamoto kubwa kwa Serikali nyingi za Kiafrika zinazotumia fedha nyingi kuagiza bidhaa mbalimbali

Miaka miwili iliyopita, Benki ya Maendeleo ya Afrika ilibainisha katika utafiti kuwa mwelekeo huu wa kuagiza bidhaa unaakisi kilichotokea miaka ya 1980 na kwamba "utegemezi wa Afrika wa chakula kutoka nje unatarajiwa kufikia dola bilioni 110 ifikapo 2025".

Hali hii ya utegemezi wa chakula, hasa kwa bidhaa za kilimo, inahangaisha mamlaka, wachumi na jamii ya wanasayansi barani Afrika.

Katika hali hii, Dk. Somé anaelezea muktadha na motisha ya kazi ya timu yake. Anaeleza kuwa lengo kuu la utafiti ilikuwa kutoa mbadala bora kwa wakazi milioni 20 wa Burkina Faso kwa kuleta zao la viazi tofauti ile iliyopo sokoni.

Kulingana na timu ya Dk. Somé, aina ya mbegu ambayo yeye na timu yake wameboresha na kuanza kulima ina faida kadhaa.

"Tuligundua kuwa aina ya viazi inayopatikana Burkina Faso ilikuwa na nyama nyeupe, aina isiyo nzuri sana kwa lishe. Kwa hivyo, tuliamua kuhakikisha watu wanakula viazi vilivyoboreshwa zaidi," Dk. M M, mtafiti mkuu wa vinasaba na uboreshaji wa mimea, anaiambia TRT Afrika.

Dk. Somé, ambaye alipewa cheo cha "Chevalier de l'ordre du mérite de l'Étalon" kwa kazi yake mwaka 2002, anabainisha kuwa utafiti wa awali ulimpelekea yeye na timu yake kufikia hitimisho kuwa ilikuwa inawezekana kuiboresha hio mbatata tamu yenye nyama nyeupe kwa kutumia mchakato maalum.

Mchakato wa Maabara

Kutokana na wazo kwamba aina mpya ya viazi vitamu inaweza pia kulimwa nchi jirani, wanasayansi wa Burkina Faso waliendesha mchakato huo wa kisayansi katika maabara.

"Tulipata mbegu kutoka Kituo cha Kimataifa cha Viazi, ambacho pia kinashughulikia viazi vitamu, na kutoka kwa wenzetu wa Afrika Mashariki. Tulijua kwamba aina hizi zimeshazoea maeneo yao ya asili kuhusu muda wa kilimo, hali ya udongo, na hali ya hewa," Dkt. Somé anaieleza TRT Afrika.

"Tulitumia mbegu za nje kama vyanzo vya vinasaba na kuviunganisha na na aina za ndani kwa matumaini kwamba vinasaba vyenye vitamini kama beta-karotini vitahamishiwa kwenye mbegu zetu."

Aina mpya zinaweza kupatikana katika fomu za kusindika, ikiwa ni pamoja na keki, na juisi. Picha: TRT Afrik

Mchakato huu ulianza mwaka 2008. Dkt. Somé na timu yake yenye watu 11 walichukua miaka sita kurekodi matokeo ya kwanza yanayojitosheleza.

Watafiti walikuwa na uwezo wa kuzalisha aina tano za viazi vitamu, ambazo ziliidhinishwa mara moja.

"Tuligundua kwamba aina za 2014 zilikuwa zimeshakubali asili ya vyanzo vyao vya vinasaba. Zilikuwa na rangi nzuri na beta-karotini ya kutosha, lakini udhaifu wao ulikuwa kwenye upinzani dhidi ya magonjwa ya virusi," anasema Dkt. Somé.

Kulingana na matokeo haya, watafiti walianza kufanya kazi kwa bidii zaidi ili kupata matokeo bora mwaka 2018.

Aina tatu mpya za viazi vitamu ziliibuka na sifa bora, sawa na hizo za 2014, pamoja na upinzani mzuri dhidi ya magonjwa ya virusi.

"Tumefikia hatua nyingine sasa kuhusu kukuza mfumo wa mbegu. Pia tumestawisha maabara kwa ajili ya utafiti zaidi. Tumeweka mfumo mzuri utakaowezesha aina hii ya viazi vitamu kulimwa kwa kiwango kikubwa," Dkt. Somé anaiambia TRT Afrika.

Wakulima wa ndani wamepewa mafunzo katika mbinu zinazofaa kwa kilimo cha aina hii mpya, na sekta imefaidika na mafunzo.

Taasisi ya Utafiti wa Sayansi na Teknolojia na idara ya teknolojia ya chakula ya nchi hiyo zimehusika katika mchakato huu.

"Ukienda Burkina Faso leo, utapata viazi vitamu vyenye rangi ya machungwa katika aina zote zilizopikwa, ikiwa ni pamoja na kroketi, biskuti, keki, na juisi. Inapotumika kutengeneza mkate, viazi vitamu hivi vinahifadhi sawa na asilimia 35 ya ngano," anasema Dkt. Somé.

Maoni kutoka kwa watu ambao tayari wameshakula aina mpya ya viazi vitamu kwa kiasi kikubwa yamekuwa chanya.

Wakulima wa eneo hilo wamefunzwa mbinu zinazofaa kwa kilimo cha aina mpya. Picha: TRT Afrika

"Ukizingatia kiasi cha shauku kilichoonyeshwa na wakulima, wanasiasa, madaktari, na wengine, tunaridhika. Karibu kila mtu anaunga mkono aina hii ya mbegu. Mtu akila tu 135g ya viazi vitamu hivi na wali kila siku, inatosha kukidhi mahitaji ya vitamini," Dkt. Somé anasisitiza.

Masuala mapya yanayofanyiwa kazi na timu ya utafiti wa viazi ni uhifadhi endelevu wa 100% bila mabadiliko ya vinasaba.

Pamoja na viazi mbatata, Dkt. Somé na timu yake ya utafiti wanafanya kazi pia kwenye mizizi kama vile magimbi, viazi vitamu, na viazi vingine ili kuboresha ladha na thamani yao lishe.

TRT Afrika