Benki kuu ya Zimbabwe imezindua "fedha mpya" imeungwa mkono na dhahabu siku ya Ijumaa.
Haya yanajiri huku ikilenga kukabiliana na mfumuko wa bei uliokithiri na kuleta utulivu wa uchumi wa nchi unaoyumba kwa muda mrefu.
"Kuanzia leo... benki zitabadilisha salio la sasa la dola ya Zimbabwe kuwa sarafu mpya, ambayo itaitwa 'Dhahabu ya Zimbabwe' (ZiG),'' gavana wa Benki ya Hifadhi John Mushayavanhu alisema alipokuwa akiwasilisha taarifa ya sera ya fedha.
Hatua hiyo inatarajiwa ''kukuza urahisi, uhakika, kutabirika katika masuala yetu ya kifedha," alisema.
TRT Afrika