Skytrax, shirika huru maarufu la kimataifa la usafiri wa anga linalotambuliwa ulimwenguni ambalo tangu 1999, limekuwa likiandaa Tuzo za Viwanja Bora vya Ndege Duniani limetoa orodha hiyo. Picha: Getty / Photo: Getty Images

1. Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Cape Town, Afrika Kusini

Kwa mujibu wa Kampuni ya mashirika ya viwanja vya ndege Afrika Kusini, "Uwanja huu unaorodheshwa kuwa uwanja wa ndege wa 3 kwa ukubwa barani Afrika.

2. Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Durban King Shaka, (KSIA) Afrika Kusini

Uwanja huu wa ndege uliopewa jina la babu wa Ufalme wa Wazulu, ni moja ya viwanja vya ndege vikubwa na vizuri zaidi Barani Afrika. Uwanja huu unaopatikana KwaZulu-Natal, una uwezo wa kuhudumia abiria milioni 7.5 kila mwaka.

3. Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa O.R. Tambo, Afrika Kusini

Uwanja huu wa ndege ulioko Gauteng, unafahamika kuwa uwanja wa ndege wa pili wenye shughuli nyingi Afrika, ukiwa na uwezo wa kushughulikia hadi abiria milioni 28 kila mwaka.

4. Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mohammed V, Casablanca, Morocco

Uwanja huu wa ndege ulioko Morocco, uliopewa jina la Mfalme Mohammed V wa Morocco, ambaye aliongoza msukumo wenye mafanikio wa uhuru wa nchi hiyo kutoka kwa utawala wa kikoloni wa Ufaransa na Uhispania, ndio uwanja wa ndege wa tatu wenye shughuli nyingi zaidi Barani Afrika.

Uwanja huu wa ndege hupokea asilimia 95% ya nishati kutoka nishati mbadala, ikiwa ni pamoja na upepo na nishati ya jua.

5. Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Sir Seewoosagur Ramgoolam SSR, Mauritius

Uwanja huu wa Sir Seewoosagur Ramgoolam kwa kifupi SSR, ulioko takriban kilomita 50 kutoka mji mkuu wa Port Louis, umepewa jina baada ya aliyekuwa waziri mkuu wa kwanza wa Mauritius na baba mwanzilishi wa Mauritius.

6. Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Marrakech Menara, Marrakech, Morocco

Uwanja huu wa ndege ndio uwanja mkuu wa kimataifa nchini Morocco, wenye uwezo wa kuwalaki zaidi ya abiria milioni 6 kwa mwaka, ikiunganisha pia ndege za ndani na za kimataifa kwenda na kuwasili kutoka mji wenye utajiri wa utamaduni wa Morocco wa Marrakech. Uwanja huu, kwa ufupi, RAK, pia una uwezo wa ajabu wa kupokea ndege 39 za kati na za masafa marefu kwa wakati mmoja.

7. Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Addis Ababa Bole, Ethiopia

Uwanja huu maarufu ulioanzishwa mnamo 1962, ndio uwanja maarufu na wenye shughuli nyingi kwa kuwahudumia wasafiri wa kimataifa nchini Ethiopia. Uwanja huu wa ndege pia una uwezo wa kuwahudumia wasafiri milioni 12.1 kwa mwaka na ni makao makuu ya Shirika la Ndege la Ethiopian Airlines.

8. Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kigali, Rwanda

Kabla ya Uviko-19, uwanja huu wa ndege wa Kigali, ulikuwa ukiwasafirisha takriban abiria milioni moja kila mwaka huku idadi hiyo ikivuka zaidi ya abiria milioni 1.5 kwa mwaka.

9. Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, Nairobi, Kenya

Uwanja huu wa JKIA, uliopewa jina baada ya rais wa kwanza wa Kenya, Mzee Jomo Kenyatta, na ulioko mji mkuu wa Nairobi, uliwapokea abiria milioni 10.2 mnamo 2022, ikiwa ni ongezeko kutoka abiria milioni 6.7 mnamo 2021, kwa mujibu wa utafiti wa takwimu za Ofisi ya Taifa ya Takwimu nchini Kenya (KNBS).

10. Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Bram Fischer Bloemfontein, Afrika Kusini

Uwanja huu wa Bram Fischer, ulioko mji wa Bloemfontein, unatoa huduma za kisasa za usafiri wa ndege kwa zaidi ya abiria 300 000.

TRT Afrika