Bei ya mafuta imepanda karibu asilimia sita katika biashara ya Asia baada ya wazalishaji wakuu wakiongozwa na Saudi Arabia kutangaza kupunguza kwa ghafla zaidi ya mapipa milioni moja kwa siku.
Kupunguzwa huko kulisababishwa na uamuzi wa Urusi wa kupanua kata ya mapipa 500,000 kwa siku, licha ya wito wa Amerika kuongeza uzalishaji.
Mkataba wa kampuni ya West Texas Intermediate ulipanda kutoka asilimia 5.74 hadi $80.01 kwa pipa, huku ule wa Brent ukipanda kutoka asilimia 5.67 hadi $84.42 kufikia Jumatatu asubuhi.
Hatua hii ya Saudi Arabia, Iraq, UAE, Kuwait, Algeria na Oman itaanza kutekelezwa kuanzia mwezi ujao hadi mwisho wa mwaka huu, na kuashiria kupungua kwa kiwango kikubwa zaidi cha pato tangu shirika la OPEC+ kupunguza mapipa milioni mbili kwa siku mwezi Oktoba.
Tangazo hilo limeleta hofu mpya kuhusu mfumuko wa bei na kuweka shinikizo zaidi kwa benki kuu za nchi mbali mbali kuongeza viwango vya riba zaidi.
"Huenda hisa hazitathamini maendeleo haya, kwa hivyo tunaweza kuwa na mwanzo mgumu wa wiki." Alisema Matt Simpson,mchambuzi mkuu wa soko wa kampuni ya City Index.
Hatua hii inatarajiwa kutikisa uzalishaji katika sekta zote za uchumi kwani mafuta ni nguzo kuu ya uzalishaji.