Rais Joe Biden atatangaza kuweka mapipa milioni 15 hatimaye katika soko kutoka hifadhi ya kitaifa ya mafuta marekani, kwa matarajio ya ongezeko iwapo bei za nishati zitapanda, afisa mkuu wa marekani alisema.
Kiasi kipya kutoka hifadhi maalum ya petroli itakua ‘inakamilisha mapipa milioni 180 kutolewa katika majira ya machipuko,’ ili kukidhi mfumuko wa bei unaosababishwa na vita vya Urusi na Ukraine, kiongozi huyo alisema Jumanne.
Amri, ambayo Biden atatangaza katika hotuba Jumatano, ina maana kwamba Rais atakua ‘anaweka wazi kuwa utawala uko tayari kufanya ongezeko maalum… mauzo msimu majira ya baridi iwapo italazimu kwa sababu ya Urusi au sababu nyenginezo zinazoleta purukushani ya mfumko wa bei,’ kiongozi huyo aliongezea.
Biden pia atasema kwamba hifadhi hiyo ya Marekani ita jazwa tena pindi bei zikifika au zikiwa chini ya dola 67 hadi 72 kwa pipa, ofa ambayo utawala unasema utaongeza uzalishaji wa ndani kwa ndani kwa kuhakiki mahitaji iwapo bei zitashuka.
WANACHAMA WA DEMOCRAT WATIZAMIA AFUENI
Shirika la magari marekani limeripoti kwamba gesi imefikia dola 3.87 kwa galoni moja, ambapo ni ongezeko kutoka mwezi uliopita wakati bei za chini ziliashiria kwa utafiti kwamba Rais na wanachama wake wanaelekeza katika afueni.
Biden amepinga sera zinazoungwa mkono na wazalishaji mafuta marekani.
Alisisitiza, ananuia kupunguza bei kwa kutoa mafuta kutoka kwa hifadhi ya kitaifa, akikashifu makampuni ya mafuta na faida zao na kunadi ongezeko la uzalishaji kutoka nchi za OPEC+ ambazo zinaegemea maslahi tofauti kisiasa, alisema Frank Macchiarola, naibu Rais wa sera,uchumi na udhibiti mambo katika taasisi ya petroli Marekani.
Biden ananuia kuachana na nishati kisukuku kabisa kwa ruwaza ya kumaliza gesi chafu mwaka 2050.
Matarajio ya kupunguzwa kwa mapipa milioni 2 kwa siku -- asilimia 2 ya ugavi duniani -- imesema ikulu ya White house kwamba Saudi Arabia imeegemea kwa Rais wa Urusi Vladimir Putin na kuahidi kulipiza kisasi kwa kupunguzwa ugavi ambao unatishia kufumiuka wa bei.
Kutolewa kwa mapipa milioni 15 hakuwezi kukidhi matumizi ya siku moja marekani, kulingana na utawala wa nishati na mawasiliano.