Waziri wa Ulinzi wa Uganda Sarah Mateke amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi, serikali ya nchi hiyo imesema.
Waziri huyo alikuwa akipokea matibabu katika hospitali moja mjini Kampala, ambapo alipelekwa asubuhi ya Jumamosi, kulingana na Waziri wa Habari wa Uganda.
"Ninasikitika kutangaza kifo cha Waziri wa Ulinzi ambaye pia alikuwa mbunge wa Kisoro. Mungu aijalie faraja familia yake na apumzike kwa amani," alisema.
Mateke aliteuliwa kama waziri wa ulinzi mwezi Aprili baada ya Rais Museveni kufanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri, akiwa amehamishwa kutoka Wizara ya Jinsia.
Pia alikuwa ni mbunge wa eneo la Kisoro.
Makamu wa Rais wa nchi hiyo Jessica alionesha kushtushwa na kifo hicho, kulingana na chapisho lililowekwa kwenye ukurasa wake wa X.
'Kifo cha ghafla'
"Nimehuzunishwa sana na taarifa za kifo cha ghafla cha Sarah Mateke. Natuma salamu zangu za rambirambi kwa Rais wa Uganda, watu wa Kisoro na wananchi wote wa Uganda," alisema.
Kulingana na msemaji wa wizara ya ulinzi, Mateke alikuwa anatarajiwa kuelekea nchini Korea Kusini siku ya Jumamosi mchana, mtandao wa New Vision.
Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Uganda Jan Sadek pia alioneshwa kusikitishwa na kifo cha waziri huyo.
"Alikuwa kiongozi aliyejitolea na mwenye nguvu katika nyanja zake zote za kisiasa na mfuasi mkarimu wa ushirikiano wa Umoja wa Ulaya na Uganda," alisema katika chapisho lake la X.