Makundi kadhaa ya waasi yamekuwa yakileta shida katika eneo la Mashariki la DRC kufuatia mapigano kati ya Jeshi la Congo na waasi wa M23 / Picha: Reuters  

Kiasi cha watu milioni 7 huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamekosa makazi kutokana na migogoro inayoendelea nchini, Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM), limesema.

Katika ripoti yake ya hivi karibuni, IOM inasema kuwa watu wapatao milioni 6.9 wamekosa makazi kati ya mwezi Juni na Agosti.

"Hali ya sasa nchini DRC sio ya kuridhisha kutokana na ukosefu wa salama," lOM ilisema chapisho lake kwenye ukurasa wa X.

Athari za vita

Kulingana na ripoti ya IOM, zaidi ya asilimia 87 ya wakimbizi walitokana na migogoro, wakati asilimia 13 walitokana na majanga ya asili.

Ripoti hiyo imeanishia maeneo kadhaa yenye wakimbizi wengi wa ndani, ikiwemo Ituri, Kivu Kaskazini, Kivu Kusini na Tanganyika.

Maeneo mengine yaliyoathirika ni pamoja na Tshopo, Haut-Lomami, Maniema, Kinshasa na Mai-Ndombe.

Makundi kadhaa ya waasi yanaendesha harakati zake mashariki mwa DRC, ambako mzozo umekuwa ukiendelea kwa miaka mingi na mapigano mapya ya hivi karibuni kati ya wanajeshi wa Kongo na waasi wa M23.

TRT Afrika