Watu kadhaa wapotea katika maporomoko ya ardhi nchini Uganda

Watu kadhaa wapotea katika maporomoko ya ardhi nchini Uganda

Taifa hilo la Afrika mashariki limekuwa likikumbwa na mvua kubwa tangu mwezi Machi.
  Juhudi za uokoaji zinaendelea kuwatafuta waliopotea katika parokia ya Buluganya. /Picha: Chama cha Msalaba Mwekundu Uganda  

Watu watano wameuawa na wengine kadhaa hawajulikani walipo kufuatia maporomoko ya udongo katika wilaya ya Bulambuli nchini Uganda kutokana na mvua kubwa, Shirika la Msalaba Mwekundu la Uganda linasema.

"Sehemu yetu ya Kukabiliana na Dharura ilitoa mwito wa dharura wa kujibu huko Buluganya, Bumasobo - Wilaya ya Bulambuli kufuatia mvua kubwa iliyosababisha maporomoko ya ardhi", walifichua kwenye Twitter siku ya Alhamisi.

Afisa wa uhusiano wa umma wa Shirika la Msalaba Mwekundu la Uganda, Irene Nakasiita aliviambia vyombo vya habari kuwa nyumba chache zilifukiwa katika tukio hilo na huduma za dharura zilikuwa zikifanya kazi na jamii ya eneo hilo katika shughuli ya uokoaji.

Idadi ya waliopoteza maisha bado haijathibitishwa huku shughuli za utafutaji na uokoaji zikiendelea. .

Uganda imekuwa ikikumbwa na mvua kubwa tangu Machi. Watu sita waliuawa mapema mwezi huu katika maporomoko ya udongo kusini magharibi mwa wilaya ya Kisoro.

Shirika la Msalaba Mwekundu la Uganda linasema maeneo mengine ya nchi yaliyoathiriwa na mafuriko na maporomoko ya ardhi ni pamoja na Kagulu, Masugu, Namakere na Namagugu

TRT Afrika