Watu wanaodhaniwa kuwa ni wenye imani kali wamevamia kijiji kimoja nchini Uganda, na kuua watu wanane, akiwemo mtoto mdogo, mamlaka za nchi hiyo zimesema siku ya Jumatano.
Tukio hilo limetokea siku ya Jumanne usiku katika kijiji cha Mizizi A, kilichopo wilaya ya Kagadi, magharibi mwa Uganda. Kulingana na Jeshi la Polisi, watu wengine wanane walijeruhiwa katika tukio hilo.
"Taarifa za awali zinaonesha kuwa wafuasi wa kikundi hicho, waliivamia familia moja na kuanza kuwakatakata," Jeshi la Wananchi la Uganda limesema.
Vikosi vya usalama vikiwemo kutoka jeshi na polisi vilikuwa eneo la tukio "kuwasaka wahalifu huku uchunguzi ukiendelea ili kupata maelezo zaidi kuhusu kikundi hicho", lilisema UPDF.
Watoto ni kati ya waliouwawa
Wanne kati ya waliouawa walikuwa na umri wa chini ya miaka 13, akiwemo mtoto wa miaka mitatu, polisi wamesema.
Kulingana na Polisi, watuhumiwa wawili wa tukio hilo waliuawa na vikosi vya usalama.