MONUSCO imetumwa mashariki mwa Kongo tangu kuchukua nafasi ya operesheni ya awali ya Umoja wa Mataifa mwaka 2010./ Picha : Reuters 

Mkuu wa ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo alisema wafanyakazi wake na magari yalishambuliwa katika mji mkuu Kinshasa siku ya Jumamosi huku mzozo wa usalama wa mashariki ukichochea zaidi chuki dhidi ya ujumbe huo.

''Idadi ya magari ya misheni hiyo yalichomwa,'' alisema mkuu wa MONUSCO Bintou Keita katika chapisho la mtandaoni.

"Ninalaani vikali mfululizo wa mashambulizi," alisema

Umati wa watu wakiwa kwenye pikipiki walikusanyika katika wilaya ya Gombe kando ya mto, ambako misheni ya Umoja wa Mataifa inayojulikana kwa jina la MONUSCO na balozi nyingi zinapatikana. Walichoma matairi na kuwashambulia watu, mwanidshi wa Reuters alisema.

Ubalozi wa Ivory Coast pia ulisema moja ya magari yake yameharibiwa mjini Kinshasa, na kuelezea mashambulizi ya kiholela dhidi ya magari ya balozi na mashirika ya kimataifa.

Polisi wa Kinshasa na serikali hawakujibu ombi la maoni.

Lawama kwa kikosi cha MONUSCO

Kuzidi mashambulio ya kundi la waasi la M23 ambalo linatishia mji wa kimkakati wa mashariki wa Goma katika mkoa unaokumbwa na vita wa Kivu Kaskazini kumezidisha mzozo wa kiusalama na wa kibinadamu uliodumu kwa miongo kadhaa.

Mapigano kati ya waasi, wanajeshi na makundi ya kujilinda ambayo yanaunga mkono jeshi yameongezeka katika wiki za hivi karibuni, na kuwalazimu zaidi ya watu 135,000 kukimbilia maeneo yanayodhaniwa kuwa na usalama zaidi karibu na Goma, shirika la Umoja wa Mataifa la kutoa misaada ya kibinadamu OCHA lilisema Alhamisi.

MONUSCO imetumwa mashariki mwa Kongo tangu kuchukua nafasi ya operesheni ya awali ya Umoja wa Mataifa mwaka 2010.

Majukumu yake ni pamoja na kuunga mkono juhudi za serikali ya Kongo kuleta utulivu katika eneo hilo, lakini katika miaka ya hivi karibuni imekuwa ikikabiliwa na wakati mwingine maandamano ya vurugu yanayohusishwa na dhana ambayo haijafanya vya kutosha kukomesha umwagaji damu wa mashariki.

TRT Afrika na mashirika ya habari